
KATIKA kuendeleza dhamira yake ya kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii, kampuni ya kubahatisha nchini, Meridianbet, imefanya zoezi maalum la ugawaji wa vyakula kwa familia zenye uhitaji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Zoezi hili ni sehemu ya mpango wa kampuni wa Corporate Social Responsibility (CSR) unaolenga kuhakikisha kuwa jamii, hasa zile zinazopitia changamoto za kiuchumi, zinapata msaada wa msingi unaoweza kuboresha ustawi wa maisha yao.
Meridianbet imejitokeza kuhakikisha kuwa hakuna familia inayolala njaa. Kupitia mradi huu, mamia ya familia zimepatiwa vifurushi vya chakula vinavyohusisha bidhaa muhimu kama mchele, unga, sukari, maharage, mafuta ya kupikia, sabuni, na bidhaa nyingine za matumizi ya nyumbani.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, mwakilishi wa Meridianbet alisema “Tunatambua changamoto nyingi zinazowakabili wananchi katika kipindi hiki cha maisha. Kama kampuni yenye moyo wa kusaidia jamii, tumeona ni muhimu kuchangia katika kuhakikisha familia zenye uhitaji zinapata angalau mahitaji ya msingi ya chakula. Huu ni mwendelezo wa juhudi zetu za kuhakikisha jamii inapata faraja na msaada wa kweli.”
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Kwa upande wao, baadhi ya wanufaika walionyesha shukrani zao kwa msaada huo, wakieleza kuwa umefika kwa wakati muafaka na kuwapa tumaini jipya katika wakati ambao hali ya kiuchumi imekuwa ngumu.
Zoezi hili pia liliambatana na ziara fupi ya kutembelea baadhi ya kaya zenye uhitaji mkubwa, ambapo timu ya Meridianbet ilitaka kujionea hali halisi na kujadiliana na viongozi wa mitaa ili kujenga mpango endelevu wa kutoa misaada ya kijamii kwa siku zijazo.
Meridianbet imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo misaada kwa vituo vya watoto yatima, maboresho ya mazingira, elimu ya vijana, msaada kwa wagonjwa na vituo vya afya, pamoja na kampeni za michezo na burudani kwa ajili ya jamii.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...