SIKU ya leo Novemba 28, 2025 Meridianbet imeendelea kuthibitisha kuwa biashara inaweza kuwa daraja la matumaini kwa jamii. Kampuni hiyo imetoa mashuka mapya kwa Hospitali ya Ndumbwi, tukio lililoonesha kuwa uwekezaji katika ustawi wa jamii ni sehemu ya utamaduni wao.

Katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Afisa Habari wa Meridianbet, Nancy Ingram, alisisitiza kuwa kampuni hiyo imejenga utamaduni imara wa kujali na kusaidia maeneo yenye changamoto za kijamii.

“Meridianbet imekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia jamii, na leo tupo hapa Ndumbwi kama sehemu ya dhamira yetu endelevu ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, hasa katika sekta nyeti ya afya.”

Utajiri wako upo kwenye michezo ya Kasino siku ya leo ingia na ucheze Poker, Keno, Roulette, Aviator, Superheli na ukusanye maokoto zaidi na zaidi. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz kubashiri mechi zote.

Uongozi wa Hospitali ya Ndumbwi ulipokea msaada huo kwa shukrani, wakieleza kuwa mashuka hayo yatakuwa suluhisho muhimu katika kuimarisha huduma za wodi na kuongeza faraja kwa wagonjwa.

“Msaada huu umefika wakati muafaka, na tunathamini sana kujali kwenu jamii yetu. Mashuka haya yataboresha hali ya wodi zetu na huduma tunazotoa,” alisema mmoja wa wakurugenzi wa hospitali.

Kwa miaka kadhaa sasa, Meridianbet imekuwa ikitoa mchango mkubwa kupitia miradi yao ya Corporate Social Responsibility (CSR), ikiwemo misaada kwa vituo vya watoto yatima, shule, vikundi vya kijamii, na hospitali. Msaada wa Ndumbwi unachagiza rekodi hii njema, ukionyesha kuwa jitihada za kampuni hiyo hazina mipaka linapokuja suala la kugusa maisha ya watu.

Mwisho, kupitia mradi huu, Meridianbet imeonyesha kuwa mafanikio ya kampuni hayapaswi kutenganishwa na ustawi wa jamii inayoujenga. Kwa kutoa mashuka kwa Hospitali ya Ndumbwi, kampuni imetuma ujumbe mzito kwamba kujenga jamii yenye afya bora na matumaini mapya ndiyo jambo ambalo linapaswa kupigiwa chapuo na kila mdau wa maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...