CHUO Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Mbeya, kimekamilisha ujenzi wa zahanati ya kisasa iliyogharimu shilingi 465,706,251.70, ambayo sasa imeanza kutoa huduma za afya kwa wana-Mzumbe pamoja na wakazi wa jamii inayozunguka chuo hicho.
Akizungumza Novemba 27, 2025 katika mahafali ya 24 ya Ndaki hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, amesema kukamilika kwa zahanati hiyo ni hatua muhimu katika kuboresha ustawi wa wanafunzi na watumishi wa chuo.
Prof. Mwegoha amesema huduma hizo zitarahisisha upatikanaji wa matibabu, hatua itakayowasaidia wanafunzi kutumia muda zaidi kwenye masomo yao bila usumbufu wa kufuata huduma za afya nje ya chuo.
“Na hii itawapa nafasi ya kujikita zaidi kwenye masomo yao na kuboresha ustawi wao, jambo muhimu kwa mafanikio ya kitaaluma,” amesema Prof. Mwegoha.
Aidha, Mhadhiri huyo amebainisha kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kinaendelea na jitihada za kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike. Taarifa zinaonyesha kuwa hadi sasa, jumla ya shilingi 154,813,972.00 zimekusanywa kupitia njia mbalimbali za michango.
Kati ya kiasi hicho, shilingi 99,478,972.00 zimetumwa kupitia namba maalumu ya malipo, huku shilingi 55,335,000.00 zikichangwa kupitia Baraza la Wahitimu.
Prof. Mwegoha alisema chuo kimejipanga kutenga bajeti kila mwaka wa fedha ili kuongeza nguvu kwenye utekelezaji wa mradi huo muhimu, hatua itakayosaidia kuanza rasmi mwaka wa fedha 2026/2027
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo, Dkt. Ali Mohamed Shein, mewapongeza na kuwasisitiza juu ya uadilifu na uchapakazi kwa ajili ya maendeleo binafsi na ya jamii yote kama ilivyo kauli mbiu ya Chuo Kikuu Mzumbe, "Tujifunze Kwa Maendeleo ya Watu".
Aidha, Bw. William Kibona, Mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya mwenye GPA ya 4.7 Shahada ya Uhasibu na Fedha, ameeleza kuwa ili kufanikiwa yapaswa kumtanguliza Mungu kwanza na kuwa na nidhamu katika kutimiza malengo.
Pia, ameushukuru uongozi wa Ndaki ya Mbeya chini ya Rasi wa Ndaki hiyo, Prof. Henry Mollel kwa malezi mazuri ya kitaaluma na uendeshaji yaliyochangia mafanikio yake na wahitimu wote.
Wazazi, walezi wa wahitimu na wageni waalikwa wamesifia Sherehe ya Mahafali ya 24 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya, kwa kuongeza idadi ya wahitibu bora jambo linalodhihirisha kuwa Chuo Kikuu Mzumbe ni chuo bora zaidi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...