Na Mwandishi Wetu, Karatu

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea na programu ya kutoa elimu ya uhifadhi shirikishi na kuhamasiha utalii wa ndani kwenye shule mbalimbali ambapo leo tarehe 20 Novemba, 2025  watumishi wa Mamlaka hiyo wametembelea Shule ya Sekondari Banjika iliyopo Karatu  Mkoani Arusha.

Katika ziara hiyo, wataalam wa uhifadhi na utalii walitoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi, vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro, pamoja na nafasi ya wanafunzi  kuwa mabalozi wa utalii na uhifadhi ikiwemo kuanzisha klabu za uhifadhi wa mazingira. 

Akizungumza katika ziara hiyo, Afisa Uhifadhi Mkuu- Masoko  Bw. Michael Makombe, amesema  mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wanafunzi kuhusu masuala ya utalii na uhifadhi, ili wawe mabalozi kulinda mazingira na kutangaza vivutio vya Tanzania.

“Wanafunzi ni wadau muhimu katika shughuli za uhifadhi, mazingira na utalii, Ngorongoro  tumekuwa tukigawa miche ya miti kwenye shule za karatu, Monduli, Arusha, Mbulu na maeneo mengine nchini kama sehemu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira, wanafunzi kujua umuhimu wa uhifadhi na vivutio vya utalii vilivyopo ngorongoro ili waendelee kuwa mabalozi wetu katika maeneo wanayokaa” alisema Makombe.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Banjika Mwalimu Ritha Uwo ameeleza kuwa  miti yote iliyopandwa katika shule hiyo  kuanzia 2005 imetolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuomba Uongozi wa Mamlaka hiyo kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi na utalii kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ambao hupelekea elimu hiyo kwa wazazi wao wanaporudi nyumbani na hivyo kuhamasisha utalii wa ndani na utunzaji wa mazingira.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...