Belinda Joseph- Ruvuma.

Ujenzi wa Barabara ya Songea–Lutukira yenye urefu wa Km 95.1 pamoja na Bypass ya Songea yenye Km 16, unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma, mradi huu mkubwa wa miundombinu unalenga kuboresha huduma za usafiri, kuongeza usalama wa watumiaji wa barabara na kupunguza ajali.

Pamoja na hilo, barabara hiyo mpya inatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kufungua shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazotegemea usafiri, Miundombinu iliyoboreshwa itapunguza gharama za uendeshaji wa vyombo vya moto na kuimarisha uhusiano wa kibiashara na mikoa jirani pamoja na nchi jirani.

Katika kikao cha wadau wa Mkoa wa Ruvuma cha kukusanya maoni juu ya mapitio ya usanifu wa mradi huo,  kimefanyika Novemba 25, 2025 katika ukumbi wa Songea Club Manispaa ya Songea,  Mkuu wa Kitengo cha Planning kutoka TANROADS Ruvuma Mhandisi Rubara Marando, akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya mradi huo amesema kikao hicho ni muhimu kwa kuwawezesha watumiaji na wanufaika kutoa maoni yao.

Mhandisi Marando amebainisha kuwa barabara hiyo itakuwa na mgawanyo maalum wa matumizi, ikijumuisha uwepo wa vituo vya mabasi katika kila mji, maeneo ya shule, vituo vya biashara na maeneo ya kuegesha malori kwa muda mfupi na mrefu. Aidha, njia za waenda kwa miguu zitajengwa pembeni mwa barabara, sambamba na barabara za malori katika maeneo ya milima na barabara za pembezoni (service roads) kwa maeneo ya mijini.

Kwa upande wa usalama, amesema kuwa makutano salama na ya kuvutia yatapangwa kulingana na mahitaji ya kila sehemu, Vibao vya usalama na taarifa vitafungwa, pamoja na matuta kwa ajili ya kudhibiti mwendokasi, Kutenganishwa kwa njia za magari na waenda kwa miguu kutaimarisha usalama zaidi, huku taa za barabarani zikiwekwa katika maeneo ya mjini.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Salehe Juma, alieleza kuwa mradi huo tayari ulitakuwa kuwa umeshaanza kwani fedha zimeshatengwa kwaajili ya ujenzi huo huku utekelezaji unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, alisema vyombo vya ulinzi vina wajibu wa kulinda miundombinu ya mradi dhidi ya vitendo vya uharibifu, pia aliwataka viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani ili kudumisha utulivu na kuzuia wizi wa miundombinu.

Mradi wa Songea–Lutukira ni sehemu ya mradi mkubwa wa Makambako–Songea wenye jumla ya Km 295. Mradi huo umegawanyika katika vipande vitatu: Makambako–Lwangu Km 100, Lwangu–Lutukira Km 100 na Lutukira–Songea Km 95.

Aidha, mradi unatarajiwa kufungua fursa za ajira kwa wakazi wa maeneo mbalimbali na kuongeza soko la bidhaa kwa watekelezaji wa mradi, hivyo kuwa chanzo cha kuinua kipato cha jamii.


Barabara inayotumika kwa sasa ilikamilika mwaka 1986, ikiwa na umri wa miaka 39. Wakati huo idadi ya magari ilikuwa ndogo, na muda wa uhai uliopangwa wa barabara hiyo ulikuwa miaka 25, ambayo tayari imepitwa na wakati. Hivyo, ujenzi wa barabara mpya ni muhimu ili kukidhi mahitaji ya sasa ya usafiri na maendeleo ya kiuchumi.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...