Jamii Wilayani Lindi imehamasishwa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ikiwemo miradi ya elimu ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa jamii husika.
Mkuu wa Wilaya ya hiyo Victoria Mwanziva ametoa hamasa hiyo Disemba 4,2025 aliposhiriki na wananchi wa Kata ya Nahukahuka, Kijiji cha Nahukahuka B- zoezi la kujitolea uchimbaji wa msingi wa Shule ya Msingi na Awali Nahukahuka B Halmashauri ya Mtama.
Ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wananchi wa nahukahuka kwa majitoleo yao na kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo huku baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi hilo wakimshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Elimu wakieleza kuwa mradi huo utakuwa mkombozi kwa Kata ya Nahukahuka.
Shule ya Msingi na Awali Nahukahuka B- imepokea Jumla ya fedha Shilingi Milioni 314- ambazo ni fedha za kutekeleza Ujenzi wa Vyumba 6 vya Madarasa, Jengo la Utawala na Matundu 12 ya Vyoo.



.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...