NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Diwani mpya wa Kata ya Pangani kupitia tiketi ya chama chamapinduzi (CCM) Mhe. John Katere amesesema kwamba lengo lake kubwa ni kuendeleaa kushirikiana na serikali ya awamuii ya sita katika kuhakikisha anasimamia na kuitekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi.

Katere ameyabainisha hayo katika mahojiano maaalumu mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kikazi ya Mkurugenzi mtendahi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr. Rogers Shemwelekwa ambayo ililenga kutembea na kukagua na kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleoa katika Kata ya Pangani.

Diwani huyo amempongeza kwa dhati Mkurugenzi huyo kwa kufanya ziara ya kikazi katika baadhi ya maeneo ikiwemo kutembelea baadhi ya miradi katika nyanja ya elimu, miundombinu ya barabara pamoja na kuweza kupata fursa ya kuzungumza na watendaji kuhusiana na suala zima la usimamizi wa fedha zinazotolewa katika miradi ya maendeleo.

Katere amebainisha kwamba ameyapokea maagizo yote ambayo yametolewa na Mkurugennzi huyo na kwamba anahakikisha anakwenda kuyafanyia kazi kwa bidii ikiwemo suala zima la usimamizi mzuri wa fedha ambazo zinatolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.

"Kwa kweli nipende kuchukua fursa hii kumshukuru kwa dhati Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kwa kuweza kufanya ziara katika kata ya Pangani na hii kiukweli imetupa faraja kubwa mno na kuweza kutukumbnusha kuendelea kuwatumikia wananchi ikwa sambamba na kusimamia vem matumizi ya rasirimali za fedha ambazo zinatolewa kwa ajili ya miradii,"alisema Diwani huyo.

Aidha Katika hatuua nyingine amempomgeza Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya, elimu, miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyingine za kijamii.

Awali Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr. Rogers Shemwelekwa akiwa katika ziara hiyo amewakumbusha watumishi na watendaji kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa bidii ikiwemo kuweka misingi kizuri ya kusimamia fedha ambazo zinatolewa na seriukali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Dr. Shemwelekwa amebainisha kwamba lengo kubwa la serikali ni kuwahudumia wananchi wake ikiwa pamoja na kutatua changamoto mbali mbali amabzo zinawakabili hivyo suala la kusimamia fedha ni jambo la msingi kwenda ili miradi ambayo imepangwa iweke kukamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa.

Ziara ya kikazi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha iliyopo Mkoa wa Pwani katika kata ya Pangani imeweza kutembnelea na kugagua katika baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, miundombinu ya barabara.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...