Asema Rais Dkt. Samia ni kiongozi anayetekeleza miradi inayotoa majawabu ya kero za Watanzania.
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 19, 2025 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi iliyopo Kilwa Mkoani Lindi.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, Dkt. Mwigulu amesema kuwa bandari hiyo ni mojawapo ya miradi mingi inayofafanua kauli za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alizozitoa baada ya kuapishwa za kusimamia utekelezaji wa miradi inayotoa majawabu ya kero za Watanzania.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato na kubadili maisha ya Mtanzania pamoja na kuongeza pato la Taifa. “Rais Dkt. Samia ni kiongozi ambaye anatekeleza miradi inayotoa majawabu ya kero za watanzania”
Ameongeza kuwa ili kuhakikisha mradi huo unafanya vizuri Rais Dkt. Samia ameahidi kununua meli 5 za uvuvi. “Tanzania inakwenda kuandika historia mpya kwenye sekta ya uvuvi, Rais Dkt. Samia aliahidi kuendeleza miradi iliyoanzishwa na watangulizi wake na mmoja wapo ni wa Bandari ya Uvuvi iliyopo wilayani Kilwa."
Mradi huo ambao umefikia asilimia 90 ya ujenzi wake umegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 280.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...