Watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na wenzao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), leo 23 Desemba 2025, wamekutana na kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa utendaji hususani katika usimamizi wa masuala ya kikodi yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa na EWURA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bwana Gerald Maganga, amesema EWURA ni mshirika mzuri katika kuisaidia TRA kutekeleza wajibu wake wa usimamizi wa kodi nchini.
“Ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizi mbili, utatupeleka mbele, tuudumishe na tusimamie utekelezaji wa makubaliano yetu,” alisema.
Meneja wa TRA mkoa wa Dodoma, Bwana Pendolake Elinisafi, ameishukuru EWURA kwa kuipatia TRA ushirikiano mzuri, na kuahidi kuuendeleza ili kuweka msingi imara wa mafanikio ya taasisi hizo mbili na taifa kwa ujumla.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...