Na Munir Shemweta, WANMM MASASI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amesema wizara yake haitaki watumishi wa sekta ya ardhi kuwa sehemu ya migogoro ya ardhi nchini.

Mhe. Dkt Akwilapo ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Desemba 2025 wilayani Masasi wakati alipowasili wilayani Masasi na kupokelewa kwa mara ya kwanza tangu ateuliwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

"Kuanzia sasa hatutaki mtumishi wetu awe sehemu ya tatizo tukigundua wewe mtumishi wa sekta ya ardhi umekuwa sehemu ya tatizo basi wewe siyo mfanyakazi wetu na hilo tutalisimamia". Amesema

Amebainisha kuwa, matatizo ya ardhi yapo na yanatengenezwa na watumishi wa sekta ya ardhi pamoja na wananchi ambapo ameweka wazi kuwa, matatizo yaliyotengenezwa basi wizara yake itayatatua.

"Hatupendi kufukuza kazi watumishi maana tunajua kila mfanyakazi anategemewa na kumfukuza itakuwa kitu cha mwisho lakini kuna mahali inabidi sheria ifuate mkondo wake.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo yupo wilayani Masasi mkoa wa Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine atakutana na wananchi wa jimbo lake kwa lengo la kusikiliza na kizitafutia ufumbuzi changamoto mablimbali jimboni humo.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakati alipowasili wilayani Masasi na kupokelewa kwa mara ya kwanza tangu ateuliwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.


Sehemu ya wanachama wa chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo alipowasili wilayani Masasi na kupokelewa kwa mara ya kwanza tangu ateuliwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akisalimiana na wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakati alipowasili wilayani Masasi na kupokelewa kwa mara ya kwanza tangu ateuliwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akipokelewa na vijana wa Chama cha Mapinduzi wakati alipowasili wilayani Masasi na kupokelewa kwa mara ya kwanza tangu ateuliwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...