Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt Hatib Kazungu ametoa Rai kwa Uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)Tawi la Dodoma kuendelea kutengeneza Mashirikiano na Mahusiano kwa nchi jirani,Taaisisi na hata Wadau wa Sekta ya Elimu kwa Maslahi mapana ya Taifa.

Kwa kusema kuwa Elimu inayotolewa na Chuo hicho cha Usimamizi wa Fedha itaendelea kupanda si nchini tu bali duniani kama dira na dhima inavyoelekeza na kuendelea kuimarika kwa mashirikiano pamoja na dhamira njema za Chuo hicho.

Dkt Kazungu ameyasema hayo mapema leo hii Jijini Dodoma Desemba 13,2025 wakati akimwakikisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule katika Mahafali ya 51 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM).

"Natoa Rai na kusisitiza kuwa endeleeni kutengeneza mahusiano,mashirikiano na nchi jirani pamoja na Taasisi nyingi zaidi za ndani na nje ya nchi pamoja Wadau wa Sekta ya Elimu kwa maslahi ya Taifa letu na kufanya dhamira njema ziweze kuimarika".

Aidha amesema kuwa Serikali inaahidi kuendeleza Ushirikiano na IFM katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo za ukosefu wa eneo la kutosha kwa chuo hicho lakini pia ukosefu wa hosteli kwa wanafunzi,na kuwa watakaa kwa pamoja kuona namna ya kutatua changamoto hizo lengo ikiwa ni kuona Chuo kinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa umahiri na kwa weledi mkubwa kama ilivyoainishwa katika Sheria na Miongozo mbalimbali inayosimamia Chuo hicho.

Pia Dkt Kazungu akito Wito kwa Wahitimu wa Chuo cha IFM amewaambia kuwa jamii ya Tanzani inategemea sana kutoka kwao utendaji bora,uadilifu,uzalendo na ufanizi zaidi katika fani zao,hivyo wakaoneshe ujuzi na ubunifu katika kazi zao na Mazingira yanayowazunguka.

"Sasa kwenu Wahitimu, jamii ya Tanzania inategemea sana kuona kutoka kwenu utendaji bora zaidi,uadilifu,uzalendo na mnaofanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi katika fani zenu hivyo tunatarajia kuona mkionesha ujuzi wa hali ya juu na ubunifu katinakazi zenu baada ya kupata Elimu hii".

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha IFM Prof. Emmanuel Mjema amesema kuwa Baraza hilo limeendelea kuisimamia menejimenti ya Chuo katika mwaka wa masomo 2024/25 katika kutekeleza Sheria,Sera na Miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali kuonesha kwamba Chuo kinaendeshwa kwa kufuata Sheria,Taratibu,Kanuni na Miongozo ya Serikali.

Hivyo katika kutekeleza hilo Baraza la Chuo limesimamia ubora na uboreshaji wa Mitaala iliyopo ili kuendana na mahitaji ya Soko,mabadiliko ya Teknolojia na kuendelea kukidhi mahitaji ya ndani na nje kwa viwango vya juu jambo ambalo linajidhihilisha katika mitaala hiyo.

Naye Mkuu wa Chuo hicho cha Usimamizi wa Fedha Prof Josephat Lotto amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa mafanikio ya kuanzishwa kwa mifumo ya kufundisha kwa Tehama chuoni hapo lakini Chuo hicho bado kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuwa na sehemu ya kuaminika katika utoaji huduma kwani bado wamepanga,lakini ukosefu wa Hosteli na upungufu wa Wafanyakazi.

Jumla ya Wahitimu 138 wametunukiwa Tuzo zao katika kozi 10,wanaume wakiwa 86 sawa na asilimia 62 na Wanawake 52 sawa asilimia 38 na hao ni kutoka Kampasi ya Dodoma na baadhi ya wanafunzi kutoka Kampasi ya Dar es Salaam.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...