MSIMU huu wa EPL wa 2025/26 umeanza vibaya kwa bingwa mtetezi Liverpool baada ya kuwa na matokeo ambayo hayaridhishi huku bado watu wakijiuliza kama anaweza kutetea taji lake msimu huu.

Msimu wa 2025/26 wa Ligi Kuu ya Uingereza yaani (EPL) umeibuka kuwa mmoja wa misimu yenye ushindani mkubwa katika historia ya Liverpool FC kwani huu umekuwa sio msimu mzuri kwao mpaka sasa walipofikia kwani mataokeo ambayo wamekuwa wanayapata hayaridhishi kabisa.

Licha ya kufanya usajili wa wachezaji wenye majina makubwa kama Florian Wirtz, Jeremy Frimpong, Alexander Isak, Ekitike na wengine kibao na kumuachilia beki wao Trent timu yao imezidi kudorora kwa kupata vipigo vya maana msimu huu.

Licha ya Liverpool kuanza vyema kwenye ligi msimu huu wakitaka kutetea taji lao msimu huu mbele ya kocha mkuu Arne Slot, mambo yamekuwa sio hivyo ambavyo walitarajia kwani mfungaji bora wao na pia wa ligi Mohamed Salah ameshuka kiwango kitendo ambacho kimefanya kocha asimpe nafasi ya kuanza kikosini na kupelekea tetesi za kuwa huenda akatimkia Saudi Arabia.

Tengeneza pesa na michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Mohamed Salah anaenda kushiriki michuano ya AFCON akiwa na Egypt hivyo nafasi yake itachukuliwa na wachezaji wengine waliyopo. Bado watu wanajiuliza kama mchezaji huyo anaweza akarejea kikosini hapo au ataondoka kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Liverpool mpaka sasa kwenye msimamo wa ligi wanashika nafasi ya 9 wakiwa wameshinda mechi zao 7 wakitoa sare 2 na kupoteza mechi zao 6 huku wakiwa na pointi 23, nyuma pointi 10 kwa vinara wa ligi. Pia Jogoo huyo wa Anfield msimu huu kwenye mechi zile kubwa ameshinda mechi moja pekee nayo ni dhidi ya Arsenal.

Kwenye mechi 5 za EPL mpaka sasa ameshinda mechi 1 pekee huku mjadala ukiwa ni mkubwa shida iko wapi kwa mabingwa watetezi hawa wa EPL?. Ni kocha aua wachezaji wamechoka, lakini mbona kuna ongezeko kubwa la wachezaji kwenye dirisha kubwa la usajili?

Kwenye UEFA kule nako bado wanajikokota kwani mpaka sasa wana pointi 9 kwenye mechi 5 huku wakipoteza mechi kubwa pia ikiwemo ile na Galatasaray, PSV, na mechi ijayo atamenyana dhidi ya Inter Milan kule ugenini. Je Liver anaweza kushinda mechi hiyo?.

Licha ya mwenendo usio ridhisha wa klabu hiyo, bado ina nafasi ya kutetea mataji yao chini ya kocha Slot kama hili la EPL, UEFA na mengine mengi. Lakini je sasa wazidi kuwa na Slot au waongeze nguvu kikosini msimu huu kwenye dirisha dogo?. Endelea kufanya ubashiri na Meridianbet ujiweke kwenye nafasi ya kuibuka Milionea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...