MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 14 Desemba 2025.

Dkt Kikwete amepokewa uwanjani hapo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolijia Profesa Adolf Faustine Mkenda na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Fatma Mwassa na viongozi wengine mbalimbali na wananchi.

Dkt. Kikwete yupo mkoani humo kushiriki katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkoani Kagera, itakayofanyika kesho tarehe 15 Desemba 2025. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Balozi Emmanuel Nchimbi, ambaye tayari amewasili Bukoba mapema asubuhi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...