Kilosa, Tanzania – Wakulima wa Wilaya ya Kilosa wamekabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki, baiskeli, simu janja na paneli za sola, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya “Vuna na Mixx” inayolenga kutambua na kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidigitali katika sekta ya kilimo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka, ambaye alikuwa mgeni rasmi, pamoja na viongozi wa Serikali, AMCOS, wadau wa kilimo, na wawakilishi wa Kampuni ya Yas na Mixx.

Akihutubia katika tukio hilo, Mheshimiwa Shaka aliipongeza Mixx kwa kuendeleza ubunifu wa huduma za kifedha unaowafikia moja kwa moja wakulima na kuongeza ufanisi katika sekta ya kilimo. Alisema kuwa kampeni hii imekuwa chachu ya kuwahamasisha wakulima kufanya kazi kwa bidii, kutumia teknolojia na kujihakikishia usalama wa malipo yao.

“Mchanganuo wa takwimu unaonesha wazi kuwa Kilosa ni wilaya muhimu hapa nchini kwenye suala zima la chakula hapa nchini. Zaidi ya salilimia 75 ya wakazi wetu wanajihusisha na kilimo, na zaidi ya tani 400,000 huzalishwa kila mwaka. Mixx by Yas imekuja kuongeza thamani katika mnyororo huu kwa kuweka mifumo salama ya malipo na huduma zinazomwezesha mkulima,” alisema.

Shaka aliwataka wakulima kuendelea kutumia mifumo ya malipo ya kidigitali ili kupunguza upotevu wa fedha, kuepuka safari ndefu za kufuata malipo, na kuongeza uwazi katika miamala. Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kama Mixx na Yas katika kuongeza tija, kupunguza changamoto za soko na pembejeo, pamoja na kuimarisha uchumi wa kilimo.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni, Meneja wa Biashara – Mixx, Kanda ya Pwani Kaskazini, Ndugu Anwar Kisesa, alisema kampeni ya Vuna na Mixx imeandaliwa maalum kutambua na kuthamini mchango wa wakulima ambao wamekuwa mstari wa mbele kutumia Mixx kupokea malipo yao salama na kwa wakati.

“Tunachofanya leo si kutoa zawadi tu, bali ni kuonesha kuwa mkulima ndiye injini ya uchumi wa Kilosa na Tanzania. Malipo ya kidigitali kupitia Mixx yameongeza uwazi, yamepunguza msongamano, na yamewawezesha maelfu ya wakulima kupokea fedha zao papo kwa hapo,” alisema.

Kisesa alisema kuwa zaidi ya wakala 6,000 katika mkoa wa Morogoro wamenufaika na kamisheni za miamala kupitia mfumo wa Mixx, wakati huo huo serikali ikikusanya mapato kupitia kodi za malipo ya kidigitali.

Kampuni ya Mixx imeendelea kukuza huduma zinazolenga kumwezesha mkulima, ikiwa ni pamoja na:

KilimoPesa – Mikopo nafuu ya pembejeo kama mbolea, mbegu bora na zana za kilimo.

Afya Mkulima – Huduma ya bima nafuu inayomlinda mkulima na familia yake dhidi ya gharama za matibabu.

Malipo ya Kidigitali kupitia AMCOS – Mfumo unaolinda pesa za mkulima, kuondoa upotevu na kuongeza uaminifu kati ya mkulima na chama.

Kwa mujibu wa taarifa za Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa:

• Zaidi ya 75% ya wakazi wanajishughulisha na kilimo

• Zaidi ya 400,000+ tons za mazao huzalishwa kila mwaka

• Zaidi ya 20,000+ tons za mpunga huzalishwa kila msimu

Mazao kama mahindi, mpunga, alizeti, ufuta, choroko, chia, pamba, maharage, bustani na miwa yanaongoza katika uzalishaji

Maeneo ya Kimamba, Ruaha, Dumila, Magole, Ulaya, Mvuha, Kisanga, Rudewa na mengine yameendelea kuwa kitovu cha uzalishaji wa mazao haya.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni ya Vuna na Mixx, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao na kuwaongezea nguvu katika uzalishaji.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka (kulia), akikabidhi funguo za pikipiki kwa Bw. Hassan Mbuta, mkazi wa Kilosa na mmoja wa washindi wa Kampeni ya “Vuna na Mixx”, katika hafla iliyofanyika hivi karibuni wilayani humo. Kampeni hiyo inalenga kutambua na kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidigitali kwa wakulima.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...