MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Anne Kilango, amewasihi vijana wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa Waziri wa Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka  unaotarajiwa kufanyika leo Disemba 22, 2025, katika viwanja vya Stendi ya Mabasi Ndungu.

Akizungumza kuelekea siku hiyo, Kilango alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuona umuhimu wa kuunda Wizara ya Maendeleo ya Vijana, wizara ambayo amesema itakuwa na mchango mkubwa katika kushughulikia changamoto, mafanikio na kero zinazowakabili vijana nchini.

Kilango alisema kundi la vijana ndilo kubwa zaidi nchini likiwa na takribani asilimia 64 ya Watanzania wote, hali iliyomfanya aone umuhimu wa kuwakusanya vijana wa Jimbo la Same Mashariki ili wapate nafasi ya kumsikiliza Waziri wao na kushiriki moja kwa moja katika majadiliano yanayowahusu.

Aliongeza kuwa hotuba itakayowasilishwa na Waziri wa Maendeleo ya Vijana haitahusu tu vijana wa Same Mashariki bali itakuwa ni hotuba yenye mwelekeo wa kitaifa, itakayobeba sera, mipango na fursa mbalimbali zitakazolenga kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii.

Mbunge huyo aliwataka vijana kutumia fursa hiyo kueleza changamoto zao, kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia serikali kuboresha sera na programu za maendeleo ya vijana, akisisitiza kuwa ushiriki wao ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu ya taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...