Kutokana na upungufu wa madawati katika shule ya sekondari Mvomero, Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kimetoa meza 20 na viti 20 kwaajili ya kupunguza changamoto hiyo ambayo imekuwa kero kwa wanafunzi na waalimu shuleni hapo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi madawati Mkuu wa kitengo cha masoko na mauzo kutoka Kiwanda cha sukari Mkulazi Goodluck Kway amesema msaada huo utakuwa ni chachu ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kuwataka wadau wengine kujitokeza ili waweze kushirikiana kwa pamoja kumaliza changamoto hiyo au kuipunguza kwa kiasi kikubwa kwani bado changamoto hiyo ni kubwa shuleni hapo
Awali Mkuu wa Shule sekondari mvomero Castin Damian ameeleza shule inaupungufu wa zaidi ya madawati 300 na wakati mwingine unasababisha wanafunzi kufanya mitihani wakiwa wamekaa chini.
Lakini pia Mkuu wa shule hiyo ameomba watu wa Kiwanda hicho cha Sukari Mkulazi kuendelea kuwaunga mkono na kuwasaidia pindi ambapo watahitaji msaada wao kwani bado changamoto hiyo haijaisha licha ya kupokea msaada huo ila uhitaji bado ni mkubwa.
Wakishukuru kupokea kwa madawati hayo afisa mtendaji wa kata ya mvomero na mwalimu wa shule ya hiyo pamoja na wanafunzi wameahidi kuyatunza huku bado wakiendelea kuhimiza juu ya uhitaji ambao bado ni mkubwa shuleni hapo na kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo wanahitaji kupata madawati ya kutosha ili kuweza kukidhi idadi ya wanafunzi na kuweza kusoma kwa uhuru bila changamoto yeyote.




.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...