Mabwepande, Dar es Salaam

Mbunge wa CCM Jimbo la Kawe, Geofrey Timoth,Desemba 17,2025 amefanya ziara ya kikazi katika Kata ya Mabwepande kwa lengo la kukagua na kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya kijamii na miundombinu inayoendelea kutekelezwa katika kata hiyo.

Katika ziara hiyo, Mbunge Timoth alitembelea ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na vyoo katika Shule ya Msingi Mjimpya, mradi unaolenga kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Aidha, alikagua eneo lilitengwa kwa ajili ya kujenga shule katika mradi wa viwanja vya NSSF Kinondoni – Mjimpya pamoja na eneo linalopendekezwa kujengwa shule ya msingi na sekondari katika Mtaa wa Bunju B, hatua inayolenga kupunguza msongamano wa wanafunzi na kusogeza huduma ya elimu karibu na wananchi.

Katika upande wa miundombinu, Mbunge huyo alitembelea pia barabara ya lami ya gema katika Mtaa wa Bunju B, akieleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo unaotarajiwa kurahisisha usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

Mbunge Geofrey Timoth, akiambata na Diwani wa kata hiyo Mh. Isaac  Mashimba pia alipata fursa ya kukutana na Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Mabwepande, ambapo walijadili kwa pamoja changamoto na vipaumbele vya maendeleo katika kata hiyo, ikiwemo elimu, miundombinu na huduma za kijamii. Mbunge huyo aliahidi kuendelea kushirikiana na kamati hiyo pamoja na viongozi wa serikali za mitaa katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mbunge wa CCM Mh, Geofrey Timoth alisisitiza umuhimu wa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa na kwa kuzingatia thamani ya fedha za umma.

Kwa mujibu wa ratiba,Mhe.Mbunge Geofrey Timoth ataendelea na kikao na kamati ya maendeleo kata ya Mbweni na baadae kutembelea miradi. Mh, Geofrey Timoth anatarajiwa kutembelea jumla ya kata 10 katika ziara hiyo ya ukaguzi wa maendeleo.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...