Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MBUNGE wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha ACT- Wazalendo Bakari Shingo ameamua kutenga siku tatu katika wiki kwa ajili ya kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi huku akisisitiza yeye sio Mbunge wa mitandaoni bali amejipanga kuwatumikia wananchi.

Aidha amesema kuwa yeye pamoja na madiwani wa Jimbo la Ukonga wamekubaliana kwa pamoja kuweka mipango na mikakati itakayowezesha kushirikiana kwa pamoja kuleta maendeleo ya wananchi ambao wamewachagua katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao kazi kati yake na madiwani wote wa Jimbo la Ukonga ambao kwa sehemu kubwa wanatokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo lengo la kukutana nao ni kuweka malengo yatakayowezesha kutekeleza majukumu yao .

“Uchaguzi Mkuu umeshamalizika na mimi Mbunge pamoja na madiwani tayari tumeshaapa hivyo nimeona ni vizuri kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yetu ni vema tubadilishane mawazo tuone namna gani jimbo letu la Ukonga linafanya vizuri.

“Kwahiyo baada ya kukutana tumeweka mpango kazi na tumekubaliana mambo ya msingi kwani tunajua matatizo ya wananchi wetu na tuliyojadili tutafikisha kwenye vikao husika.

“Miongoni mwa mambo tuliyojadili ni ujenzi wa miundombinu, tumejadili suala la afya ya wazee wetu ,wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.Pia tumejadili suala la kuwezesha vijana wetu na mama zetu mtaani kuweza kufanya shughuli za uwezeshaji hasa suala la ufundi stadi,”amesema Shingo.

Kuhusu wananchi watarajie nini, Shingo amesema wananchi wa Jimbo la Ukonga wamepata mbunge na madiwani ambao watakwenda kwa wananchi kuwasililiza,watakaa nao kutatua changamoto kwa pamoja.

“Wananchi watuone sisi ni sehemu yao na mimi mbunge nimetenga siku tatu kwa wiki ambayo ni siku ya Jumanne,Alhamis na Ijumaa ambazo nitakuwa nasikiliza wananchi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tisa mchana.

“Ofisi yangu pia inapatikana ofisi ya Kata ya Pugu lakini nina katibu ambaye atakuwepo kila siku kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tisa mchana,kwahiyo wananchi waje walete changamoto zao ,madiwani nao watatenga siku mbili kwa ajili ya kusikiliza wananchi .

“Tumekuwa na kikao kizuri na kwa hiyari tumekubaliana kuwatumikia wananchi na madiwani wote ambao wapo katika Jimbo letu wanafahamiana na kwa pamoja wameamua kuwa kitu kimoja katika kuwahudumia wananchi.”

Shingo amesema pia Uchaguzi mkuu ulishakwisha hivyo sasa ni wakati wa kuweka vyama pembeni ili kwa pamoja wafanye mambo ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya jimbo la Ukonga.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...