MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Nurdin  Bilal ‘Shetta’, amesema  milango ya ofisi yake  iko wazi kwa wasanii na wanamichezo  kwa jambo lolote linaliweza kusukuma mbele tasnia hiyo.

 Aidha amesema, anakusudia kuanzisha timu maalumu ya Jiji la Dar es Salaam  na kuiwezesha  kucheza ligi mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara ukiwa ni mkakati wa kuinua vipaji vya soko.

Pia, amesema anakusudia kuanzisha Bao la Meya wa Jiji la Dar es Salaam kwa timu za soka  Wilaya ya Ilala ikiwa ni kuunga mkono jiti hada za  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuinua sekta ya michezo.

Ameyasema hayo  jijini Dar es Salaam alipofungua  Bonanza la kumuenzi mdau wa soka Tarafa ya Kariakoo,  Mudrick Rashid ‘Mud Bonge’ lililofanyika katika vianja vya Mnazi Mmoja.

“Nimehudumu katika muziki kwa miaka  15.  Muziki, sanaa michezo ni kitu kimoja.Katika uongozi wangu wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam niwatoe  mashaka,  chochote mnacho kiona  kinaweza kusogeza  tasnia mbele basi ofisi yangu iko wazi,”alisema.

Ameeleza  ataangalia uwezekano wa  lutengeneza  timu ya  soka ya Jiji la Dar es Salaam  ambayo itafika hadi Ligi Kuu.

“Tutaongea na  wadau  kuhakikisha tunasapoti vipaji.Ilala ndiyo jiji linaloongoza nchi nzima kwa mapato, hivyo tunataka kuongoza hata katika michezo,”amesema  Shetta.

Amepongeza  waandaji wa bonanza hilo  la kumwenzi mdau huyo  huku akitoa wito wa uanzishaji wa vituo vya kuinua vipaji  vya wachezaji wakiwa bado wadogo.

“Tunapomuenzi   mdau huyu basi tukumbuke kuanzishe vituo  vya kulea vipaji kama wenzetu,”amesema meya huyo.

Mwenyekiti wa Chama  cha Soka Mkoa Maalumu wa Ilala (IDFA) Kondo  Mussa,  alimshukuru  Shetta kwa ahadi  hizo na kueleza  uongozi wake utaongeza chachu  kwa michezo na wanamichezo  jijini Dar es Salaam.

“Tunafarijika  na kauli  hii ya Meya kufungua milango kwa wadau wa michezo na sanaa. Ili tasnia ikue inahitaji  wadau. Tunaona mpira wa Ilala  sasa unakwenda kubadilika kwani kiongozi  ameonesha nia,”amesema.

Mratibu wa  wa  bonanza hilo  Katibu wa Veterani  Kariakoo,  Mwinyi Mudete, amesema  lilishirikisha  veterani  mbalimbali  katika kumuenzi mdau Mudi Bonge.

“Mudi  Bonge alikuwa na  mchango mkubwa katika soka hapa nchini hasa  kwa wachezaji wa  akiongoza rimu ya  Kibasila iliyokuwa na makao makuu yake  Kata ya Gerezani.  Amewatoa wanamichezo kama Credo Mwaipopo, Said Swed, Salumu Swed, Hussein Swed, Kipanya Malapa na John Mwansasu,”mesema  Mwinyi.






Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...