Na Khadija Kalili
TAASISI ya Mazingira Plus wamejipanga wanatunza mazingira kwenye maeneo ya Shule, na Taasisi kwa kuzindua mradi umaofahamika kwa jina la Taka Sifuri.

Akizungumza katika warsha ya kufungua mradi huo Jijini Dar es Salaam jana tarehe 18 Desemba 2025 Mratibu wa Mazingira Plus, Suleiman Mang’uro amesema mradi huo wa Taka Sifuri Mashuleni (Waste Zero School) una lengo la kutunza mazingira kwa kuondoa taka kwenye maeneo ya shule katika Mkoa wa Dar es Salam.

“Lengo ni kuhakikisha watoto wanasoma kwenye mazingira mazuri ili waweze kuelewa kile wanachojifunza, hivyo mradi huu umejikita kwenye utunzaji wa mazingira katika maeneo yao ili kuyafanya yawe sehemu salama kwa elimu yao,” amesema Mang’uro.

Mung’uro amesema kuwa watahakikisha taka zinapungua kwa asilimia 80 kwenye maeneo ya Shule katika Manispaa nne ambazo ni Dar es Salaam Jiji, Kindondoni, Kigamboni na Temeke.

Ametaja Shule zilizo kwenye mradi huo kuwa ni Buzza,Temeke, Mbweni, Nguva, Kigamboni na Pugu.

Akizungumza kwenye warsha hiyo iliyokuwatanisha Waalimu na Wataalamu mbalimbali, Afisa Mazingira kutoka Manispaa ya Kinondoni amesema kuwa yeye ni mdau mkubwa wa mpango wa Taka Sifuri hivyo anabeba dhima kubwa ya kuhakikisha utunzaji wa mazingira unafanikiwa kwenye Manispaa yake.

“Nina dhima ya kusambaza elimu ya utunzaji wa mazingira na zaidi kutumia taka kama fursa kwa maana zipo taka zinazoweza kutumika kwenye uzalishaji mfano mbolea,”amesema Mjabuso.

Kwa upande wake Mwalimu Kavuli Mushi wa Shule ya Sekondari ya Buza amesema kuwa kwenye warsha hiyo amepata nafasi ya kujifunza kuhusu utunzaji wa mazingira na atakuwa balozi mzuri wa mpango huo kwenye shule yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...