Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Mhe. John Mapato Meela,(Chui) ameanza rasmi majukumu yake baada ya kuwasili ofisini kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo.
Katika hatua za awali, Meela alifanya kikao kifupi na Mkurugenzi wa Halmashauri, Ndugu Shedrack Mhagama, pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Samwel Shao, kujadiliana kuhusu mwelekeo wa utendaji kazi na maeneo ya kipaumbele katika kipindi cha uongozi wake.
Viongozi mbalimbali pia walifika ofisini kwake kumpongeza na kujitambulisha, akiwemo Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Ndugu Iddy Mfinanga, na baadhi ya madiwani akiwemo Mhe. John Tarimo (Mwika Kusini) na Mhe. Onesmo Chuwa (Uru Mashariki).
Akizungumza baada ya kuwasili, Mhe. Meela alisema amejipanga kusimamia kikamilifu utekelezaji wa shughuli za maendeleo ndani ya Halmashauri na kuhakikisha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatekelezwa kwa vitendo.
“Sasa kazi imeanza. Nimeripoti ofisini rasmi leo; kilichobaki ni kuwatumikia wananchi wa Halmashauri yetu na kusimamia utekelezaji wa masuala muhimu ya maendeleo,” alisema Meela.
Amebainisha pia kuwa, pamoja na majukumu ya kila siku, kutakuwa na siku maalum mbili kwa wiki—Jumanne na Alhamisi—ambapo atakuwa ofisini kwa ajili ya kusikiliza na kuhudumia moja kwa moja kero na maoni ya wananchi.
Kwa kuanza rasmi majukumu yake, Mwenyekiti Meela ameweka wazi dhamira ya kuimarisha uwajibikaji, ushirikishwaji wa viongozi na wananchi, pamoja na kusukuma miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...