■ Ni mkakati wa kuhakikisha madini vito yanaongezewa thamani nchini.

■Ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais.Dkt. Samia katika kuendeleza mnyororo wa madini thamani.

■Waziri Mavunde amtaka mkandarasi kuongeza nguvukazi kukamilisha mradi kwa wakati.

▪️Atoa siku 7 kwa Katibu Mkuu kukutana na wakandarasi,TGC na Taasisi za serikali kwa ajili ya upatikanaji vibali muhimu vya kuendeleza ujenzi.


Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kukamilisha ujenzi wa majengo ya kituo cha mafunzo ya Uongezaji thamani madini ya vito kwa kuongeza nguvukazi na kufanya kazi kwa masaa 24 ili kukamilisha ujenzi wa jengo kwa muda mfupi.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Desemba 12, 2025 mkoani Arusha wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa kituo hicho ulioanza ujenzi rasmi ambapo katika maelekezo yake amemtaka mkandarasi kuzingatia ujenzi bora wenye kukidhi vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba.

Waziri Mavunde amefafanua kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekeleza mikakati yake kwenye mnyororo mzima wa uongezaji thamani madini ya vito kama Sera ya Madini ya Mwaka 2009 inavyoelekeza.

Sambamba na hapo, Waziri Mavunde amesisitiza kuwa, kuanza kwa ujenzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia Bunge la 13 jijini Dodoma.

Waziri Mavunde amebainisha kuwa, kukamilika kwa kituo hicho , kutaleta faida mbalimbali ikiwa pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi watakao jiunga kwenye kituo, kuongezeka kwa wataalamu wa uongezaji thamani madini ya vito, kufungua fursa za ajira kwa vijana na wafanyabiashara wa madini , pamoja na kutosafirishwa kwa madini ghafi nje ya nchi hivyo kutachagiza ongezeko la mapato kwa taifa.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mavunde ametoa siku 7 kwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini kukutana na wakandarasi ,TGC na Taasisi za serikali kwa ajili ya upatikanaji vibali muhimu vya kuendeleza ujenzi.

Kwa upande wake , Mkuu wa Wilaya Arusha Mhe. Joseph Mkude ameahidi kuendelea kufuatilia maendeleo ya ujenzi ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kama Serikali inavyotaka.

Mkude ameongeza kuwa, kukamilka kwa kituo hicho itakuwa moja ya sehemu ya uwekezaji mkubwa wa serikali husasan kwenye Sekta ya Madini mkoani Arusha.

Awali, akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi, Mkuu wa kituo cha TGC Mhandisi. Ally Maganga ameeleza kuwa, ujenzi wa majengo pacha hayo ya ghorofa 8 utagharimu Tsh Bilioni 33 na kukamilika kwake kutaongeza fursa ya vijana wengi kupata ajira kupitia ujuzi wa uongezaji thamani madini ya vito.

Naye, Meneja Mradi Mhandisi Robert Lubuva ameahidi kuhakikisha kama wakandarasi wataongeza nguvu ya rasilimali watu na vifaa ili mradi uweze kukamilika na kuwahudumia watanzania kwa wakati.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...