Na.Vero Ignatus, ARUSHA

WATAALAM wa huduma za mionzi Katika vituo vya Afya wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya mionzi ili kuepuka kiwango kikubwa kinachoweza kuleta madadhara kwa wagonjwa na wataalam husika. 
Rai hiyo imetolewa na 19 desemba 2025 Peter Pantaleo Kaimu Mkuu Ofisi ya Kanda ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kwa wataalama wa Radiolojia zaidi ya 90 waliopatiwa mafunzo yaliyoandaliwa na TAEC,na kuwataka kuwa makini na kufuata viwango vilivyowekwa kitaalam ili kulinda Afya ya wagonjwa na watoa huduma. 

Pantaleo alisema kuwa matumizi makubwa ya mionzi yanamadhara makubwa zaidi ukilinganishwa na kidogo, hivyo amewashauri wataalam hap kuwa makini zaidi, na kutambua wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum zaidi ikiwemo Kuwakinga wagonjwa pamoja na wale wanaoambatana na ndugu zao hospitalini wakati wanapopatiawa huduma za mionzi. 

"Ni Imani yetu kwamba mlichojifunza mta kwenda  kukifanyia kazi  nanyi mtakuwa mfano bora na kioo kwa wenzenu, na mafunzo haya ni muhimu sana kuhakikisha u salama wenu pamoja n wagonjwa mnaowahudumia pamoja na watu wengine waliopo mazingiellra ya hospitalini. Alisema Pantaleo. 

Mungubariki Nyaki ni mkufunzi wa mafunzo TAEC , amewataka waajiri kuendelea kuwaruhusu walaalam wa Rdijioloji kupata mafunzo kwani ni muhimu Katika Kada hiyo ili waweze kutoa huduma Bora kwa wagonjwa kwa kuzingatia matumizi sahihi ya mionzi sawa sawa na mwongozo wa kitaalam na kisheria. 

Nyaki amesema kuwa mafunzo hayo yalilenga kuwaelimisha wafanyakazi wanaofanya Katika kitengo cha Rajiolojia kwenye mahospitali yote nchini ikiwa ni pamoja na kufahamu zaidi juu ya mionzi na kazi wanazozifanya kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa, kuwa makini zaidi na wao wenyewe na wale ambao hawapo. Kwenye kitengo hicho 

"Mafunzo haya yanafanyika Kila mwisho Wa Mwaka na yanatolewa Katika awamu mbili, (a) yana kuwa ni yale ya kawaida (basic)  (b)Yale ya kuwa Katika level ya juu (advanced training program) Alisema. "

Amesema  TAEC inawataka kutambua kuwa ni sheria wafanyakazi hao  kupatiwa mafunzo kama sheria inavyoelekeza , hivyo amewashauri wale ambao hawajafika kwaajili ya mafunzo wafanye hivyo kwaajili ya kupata uwezo zaidi na kujenga ushirikiano

Amesema TAEC inahamasisha Matumizi salama ya mionzi hivyo jamii isiogope kupata huduma hiyo kwani yapo salama ni kwaajili ya matumizi ya kuchunguza magonjwa na kufanya matibabu 

Amesema changamoto Kubwa ni baadhi ya Taasisi wanamtazamo kwamba wanapoteza fedha kwa kuwaleta wapate Elimu jambo ambalo siyo sawa, 

Peter Pantaleo Kaimu Mkuu Ofisi ya Kanda ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania akizungumza na wataalam wa Radiolojia zaidi ya 90 waliopatiwa mafunzo yaliyoandaliwa na TAEC

Wataalam wa Radiolojia zaidi ya 90 waliopatiwa mafunzo yaliyoandaliwa na TAEC kutoka Katika hospitali mbalimbali nchini




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...