Na mwandishi wetu, Morocco
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande (Mb), amesema Tanzania inatumia fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), katika kujitangaza na kukaribisha wadau na wawekezaji katika sekta ya utalii ili kutanua wigo wa utalii nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Rabat, Morocco, Chande amesema kuwa jambo kubwa linalowavutia wawekezaji wengi kuwekeza katika sekta ya utalii nchini Tanzania ni kutokana na uwepo wa vivutio vingi vya utalii vilivyoibuliwa na kutangazwa vyema na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya “Tanzania: Royal Tour”.

Adha, amesema kupitia michuano hiyo inayoendelea nchini humo, serikali kupita wizara hiyo imejifunza vya kutosha uwekezaji mkubwa wa miundombunu bora, ya kisasa na kuvutia iliyofanywa na taifa hilo jambo ambalo limesaidia kupokea watalii wengi kila mwaka

“Kwa Afrika, Morocco ni miongoni mwa nchii nayoongoza kuingiza watalii wengi kila mwaka, tunatamani kuwafikia na tumeshaona baadhi ya miundombinu wanayoitumia, na sisi tunakwenda kuiboresha ya kwetu, ili kusudi tufikie idadi tuliyoelekezwa ya kufikia watalii Milion 8 ifikapo 2030, hilo linawezekana, kupitia hii AFCON tu.” Chande amesisitiza

Katika hatua nyingine Waziri Chande, ametoa wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari mbalimbali vya nchini Tanzania kuwa na vipindi mbalimbali vya kuelezea maudhui ya uhifadhi na utalii ili kutangaza fursa na mazuri yaliyomo nchini.

Waziri Chande yupo nchini humo kushiriki matukio mbalimbali ya AFCON kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu ambapo Tanzania ipo katika maandalizi ya kuwa miongoni mwa nchi mwenyeji katika mashindano ya AFCON 2027.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...