Na Mwandishi Wetu
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeshika nafasi ya pili katika tuzo ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu kwa Viwango vya Kimataifa kwa mwaka 2024 kwa Mamlaka za Udhibiti zilizoshindanishwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu nchini (NBAA)
Tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi wa Fedha CPA Pascal Karoomba Mkurugenzi wa Fedha kwa niaba yaMkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya APC Bunju Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Fedha CPA Karomba wa amesema ushindi walioupata sio rahisi kwani taasisi ni nyingi lakini bado wameendelea kuwa na ubora huku wakijipanga katika kurudi katima nafasi ya kwanza.
Amesema TASAC imeendelea kuchukua ushindi katika nafasi mbambali katika Tuzo za NBAA katika kipengele cha Mamlaka za udhibiti.
Amesema ushindi huo unaonesha rasilimali walizopewa na majukumu unaonesha jinsi ambavyo wanawajibika katika utekelezaji wa majukumu yao ambapo wamekuwa wakiyafanya kwa weledi .
Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) CPA Pascal Karomba akizungumza na Waandishi wa Habari kwa Niaba ya ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salumu kuhusiana Tuzo ya Mshindi Pili ya Uandaaji Tarifa za Fedha mwaka 2024 zinazotolewa na Bodi ya Uhasibu Nchini (NBAA) katika Hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Wakiwa katika picha mara baada ya kutangazwa washindi wa pili Tuzo za NBAA.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...