*Ni katika Mtambo wa Ruvu Chini ,DAWASA yatoa sababu kupungua kwa maji
*Aanika mikakati kukabiliana na hali hiyo, atoa neno kwa wananchi
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)imesema uzalishaji wa maji kwa sasa umepungua kutoka uzalishaji maji wa lita milioni 534.6 kwa siku hadi kufikia uzalishaji wa lita milioni 270 ambazo ni sawa na upufungu wa lita milioni 264.6 kwa siku.
Hata hivyo pamoja na upungufu huo imeeelzwa kwa hali ilivyosasa hivi sasa Mtambo wa Ruvu Chini iliyokuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 270 kwa siku hivi sasa unazalisha maji lita milioni 50 kwa siku huku Mtambo wa Ruvu Juu wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 196 ambapo sasa uzalishaji wake umepungua na kufikia lita milioni 150.
Akizungumza leo Desemba 12,2025 katika mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Mhandisi Mkama Bwire ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu DAWASA ametoa sababu za kupungua kwa uzalishaji maji na hivyo kusababisha changamoto ya uhaba wa maji katika Dar es Salaam na baadhi ya miji ya Pwani.
Ametaja sababu za uhaba wa upatikanaji wa maji ni Mvua za masika zilinyesha chini ya wastani mwezi Machi - Mei, 2025
“Kuchelewa kwa mua za Vuli zilizotarajiwa kunyesha kuanzia Oktoba - Desemba, 2025 na Mto Ruvu kuacha njia yake ya asili kwenye eneo la Kitomondo na kutengeneza mchepuko.
“Sababu nyingine ni kuongezeka kwa Joto kutoka nyuzi joto 29-31C hadi nyuzi joto 33.2-34.2 (TMA), hali hii imepelekea kina cha maji kupungua kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo maji kupotea kwa njia ya Mvuke.
Ameongeza kuwa sababu nyingine ni kuongezeka kwa shughuli za kibanadamu (kilimo, ufugaji) ndani
ya Bonde la Mto Ruvu.
Hata hivyo wakati hatua mbalimbali za muda mfupi zikiendelea kuchukua kukabiliana na hali hiyo Bwire amesema DAWASA inawaomba wananchi kuwa wavumilivu katika
kipindi hiki cha mpito na kuhifadhi maji yanayopatikana
“DAWASA na inaendelea kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na upungufu wa maji kwa lengo la kuhakikisha wananchi wote wanaendelea kupata huduma katika uwiano sawa.”
Kuhusu hatua za muda mfupi zilizochukuliwa ni kusimamisha vibali vya watumia maji wengine ili kuruhusu DAWASA kupata maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Pia DAWASA kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Pwani, Bodi ya Bonde la Wami-Ruvu, inaendelea kufanya doria kwenye eneo la Mto Ruvu kuhakikisha hakuna matumizi mengine ya maji kutoka kwenye mto.
Hatua nyingine zilizochukuliwa ni kuyagawa na kuyasimamia maji kidogo yanayoendelea kuzalishwa kwa uwiano sawa, kudhibiti mivujo ya maji kwa wakati ili kuhakikisha maji kidogo yanayopatikana yaweze kuwafikia wateja pamoja na kutoa elimu ya kuhifadhi maji na matumizi bora ya maji katika kipindi hiki
Wakati hatua zinachukuliwa za mrefu ni kuanza kwa utekelezaji wa Gridi ya maji ya Taifa, ikiwa ni pamoja na kutoa maji Mto Rufiji kuja Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Lindi pamoja na kuongeza uchimbaji wa visima vya uzalishaji maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa Mkoa wa Dar es salaam
.jpeg)





.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...