Na Diana Byera_ Bukoba.
Viongozi wa dini mkoani Kagera wameonyesha kuridhishwa na namna serikali inavyotekeleza miradi ya maendeleo mkoani humo, huku wakiahidi kuwa chanzo cha kulinda amani na utulivu pamoja na miradi hiyo.
Viongozi kutoka madhehebu yote ya dini mkoani Kagera wamekutana katika Ukumbi Mkuu wa KCU kuliombea Taifa dua na kufanya ufunguzi wa Tamasha kubwa la Ijuka Omuka, ambalo hufanyika kila mwisho wa mwaka na kuwakumbusha wadau wa mkoa wa Kagera kurudi nyumbani na kuwekeza katika nyanja mbalimbali. Tamasha hilo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa.
Kwa niaba ya makanisa ya Kipentekoste, Askofu Silvester Ayubu alisema kuwa viongozi wa dini wameridhishwa na kasi ya ujenzi wa stendi kuu ya Bukoba, soko, ujenzi wa chuo kikuu, miradi ya barabara za kimkakati, miradi ya maji, na kwa ujumla uwepo wa miradi hiyo ndio ushawishi wa pekee ulioufanya mkoa huo kuwa sehemu ya kulinda amani.
Katika utangulizi wake alisema serikali imefanya jambo kubwa kwa kuleta viongozi waliopo, na kuna mabadiliko makubwa sana ya kiutendaji, ambapo miradi mikubwa ambayo walikuwa wakiitamani kuiona katika mikoa mingine tayari wanaiona katika mkoa wa Kagera.
“Pamoja na kukutana kuomba dua hapa na kufanya ufunguzi wa Tamasha la Ijuka Omuka, yaani kumbuka nyumbani, hii ni nafasi pekee ya kushukuru serikali kwa utekelezaji. Sisi kama viongozi wa dini tunavutiwa na yanayoendelea, na ndiyo maana tumeahidi kuwa tutawaongoza vijana wetu kulinda amani katika mkoa na kujiepusha na vurugu. Na mwisho kabisa, nawaita wazawa kurudi nyumbani kuwekeza,” alisema Ayubu.
Abuddushaidi Abasi, kiongozi wa JOSUTA mkoa wa Kagera, alisema kuwa uwepo wa tamasha hili unawaweka watu pamoja, na viongozi wa dini wanatambua juhudi za Mkuu wa Mkoa za kuwaunganisha wananchi bila kujali dini, pamoja na kuleta matamasha yanayoendelea kuwajenga pamoja na kuwaimarisha.
Alisema katika kipindi hiki ambacho nchi inapitia mambo mengi, ni vyema viongozi wa dini wakapunguza matamko na badala yake wawajenge waumini wao katika mazuri na mwangaza wa kuleta amani na mshikamano.
Shekhe wa Mkoa wa Kagera kutoka BAKWATA, Haruna Kichwabuta, alisema kuwa Mkoa wa Kagera umepitia machungu mengi sana, hasa katika vita na matukio mengine yaliyopoteza amani, hivyo kupoteza amani kwa mara nyingine ni kukumbushia machungu ya miaka iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa, aliwapongeza viongozi wa dini na wananchi kwa kulinda amani ya mkoa wa Kagera, ambapo ameahidi kuwa kama kiongozi wa serikali ataendelea kupiga vita ubaguzi wa dini na atawatumikia Wanakagera kwa kusimamia miradi yote ya maendeleo iliyoanzishwa.
Katika tamasha hilo, ametoa zawadi kwa kwaya zilizoshiriki ufunguzi wa Tamasha la Ijuka Omuka, pamoja na kutoa hati mbili za viwanja vya kujenga ofisi za viongozi wa dini ili kuimarisha utendaji kazi kati yao na waumini wao.
Aidha, amewaahidi viongozi wa dini kulitangaza na kulifanya tamasha hilo kuwa endelevu, na ndilo tamasha litakalowafanya wakazi wa Mkoa wa Kagera waishio ndani na nje ya nchi kuwa sehemu moja na kufanya uwekezaji wa pamoja. Tamasha hilo limefunguliwa tarehe 18 na litatamatika tarehe 21 Desemba mwaka huu.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...