WAKAZI wawili wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shitaka moja la unyang'anyi wa kutumia silaha na kujipatia vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh bilioni 1.5 mali ya Klabu ya The Voice Tz Limited.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Desemba 11, 2025 na Wakili wa Serikali, Frank Rimoy imewataja washitakiwa hao kuwa ni Tumaini Moshi (33) na Gaspar Mmari (24) ambao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.
Akiwasomea washtakiwa hao makosa yao Wakili Rimoy alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 28915 ya mwaka 2025 wakiwa na shitaka moja moja la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Inadaiwa kuwa Oktoba 29, mwaka huu katika Klabu ya The Voice Tz Limited iliyopo eneo la Kinyerezi washtakiwa wote pamoja walifanya unyang'anyi wa kutumia silaha na kisha kuiba vitu vilivyokuwepo katika klabu hiyo.
Imeendelea kudaiwa kuwa, washtakiwa wakiwa katika eneo hilo waliiba viti 350 vya mbao na vya plastiki vikiwa na jumla ya thamani ya Sh milioni 150, vifaa vya ofisini vyenye thamani ya Sh milioni 40 na runinga 57 zilizokuwa na thamani ya Sh milioni 480.
Aidha washtakiwa wanadaiwa pia kuiba seti ya muziki yenye thamani ya Sh milioni 250, mshine ya mfumo wa malipo (POS) ikiwa na thamani ya Sh milioni 80 na vyombo vya jikoni vyenye thamani ya Sh milioni 25.
Pia inadaiwa washtakiwa waliiba vifaa vya baa vyenye thamani ya Sh milioni 15 milioni, vinywaji mbalimbali vinavyodaiwa kuwa na thamani ya Sh milioni 518 na fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 16.9 ambapo vitu vyote vina thamani ya Sh bilioni 1.5 mali Klabu ya The Voice Tz Limited.
Wakili Rimoy alidai ili kutekeleza wizi huo washitakiwa hao waliwatishia watu watatu Jammy Galus, Masoud Ahmed na Benedict Katarunga ni kwa kutumia mawe, fimbo na nondo ili waweze kujipatia vitu hivyo bila pingamizi lolote.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo aliiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.
Hakimu Nyaki aliwaeleza washtakiwa hao kuwa shtaka linalowakabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria, hivyo wataendelea kubaki mahabusu. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desema 22,mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...