Disemba 7, 2025.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Dar es salaam na Pwani kwa kutembelea matanki makubwa ya uhifadhi Maji, mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini ili kujionea hali ilivyo ya uzalishaji maji na usambazaji Ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Maji kupunguza changamoto ya upungufu wa Maji uliojitokeza kutokana na kuchelewa kwa mvua.

Waziri Aweso amewasihi Wananchi kujenga utamaduni wa kuwa na vyombo vya kutunza na kuhifadhi maji katika kipindi hiki na ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kushirikiana na wadau binafsi wenye visima vikubwa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma.

Pia Waziri Aweso ameongeza kwa kutoa maagizo kwa DAWASA kuhakikisha visima vyote vilivyochimbwa na Serikali vinaingizwa kwenye mfumo wa usambazaji ili kuongeza upatikanaji wa maji kwa Wananchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...