Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Zambia nchini, Mhe. Mathews Jere kuhusu masuala ya mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa uwili baina ya Tanzania na Zambia.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Kombo ametumia fursa hiyo kutuma salamu za shukrani kwa Rais wa Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema kwa ushiriki wake katika hafla ya kumwapisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa hotuba nzuri iliyogusa mioyo ya wengi waliofanikiwa kuisikia.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...