Dar es Salaam, 10 Desemba 2025.

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angelina Kairuki, ameipongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kuongoza katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano nchini, kuchangia mapato ya serikali na kutoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 2,000.

Pongezi hizo zimetolewa kufuatia ziara ya Waziri Kairuki katika ofisi za Airtel, ambapo alifanya mazungumzo ya kina na Menejimenti ya Airtel Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinatolewa kwa ufanisi na kupatikana kote nchini.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kairuki alisema: “Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Airtel Tanzania kuhakikisha huduma za kidijitali zinawafikia Watanzania wote mijini na vijijini. Aidha, baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na menejimenti ya Airtel zitashughulikiwa ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.”

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Charles Kamoto, ametoa shukrani zake za dhati kwa ziara hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa Airtel ndiyo kampuni ya kwanza ya mawasiliano kutembelewa na Waziri tangu uteuzi wake.“Ni heshima kubwa kwa Airtel kumkaribisha Waziri. Pamoja na kwamba tulipanga kwenda kumtembelea kwanza, yeye ameamua kuja kwetu, jambo tunalolipokea kwa shukrani kubwa. Airtel imejidhatiti kuendelea kupanua huduma za mawasiliano nchini ili Watanzania wote wafurahie mtandao bila usumbufu,” amesema Bw. Kamoto.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kairuki alipata fursa ya kujionea pia miradi mbalimbali ya CSR inayotekelezwa na Airtel Tanzania, ambayo imeendelea kuleta athari chanya kwa jamii nchini kote. Miradi hiyo ni pamoja na:

● Mpango wa Uunganishaji Shuleni – kutoa vifurushi vya intaneti bure kwa zaidi ya shule za sekondari 400 na kuwawezesha walimu wa sayansi zaidi ya 2,000 kutumia vifaa vya kidijitali kuboresha ufundishaji wa masomo ya STEM.

● Programu za Ujumuishaji Kidijitali na Uwezeshaji Vijana – kuwawezesha vijana, wanawake na wataalamu kupitia mafunzo ya ujuzi wa kidijitali na upatikanaji wa teknolojia.

● Mchango wa Maendeleo ya Jamii – kusaidia programu za afya, ustawi wa jamii na elimu ya fedha kwa makundi yaliyopo katika mazingira magumu.

Ziara ya Waziri imeendelea kuimarisha nafasi ya Airtel Tanzania kama mtoa huduma bora za mawasiliano na mshirika muhimu wa serikali katika kuendesha mageuzi ya kidijitali, kutoa ajira na kuchochea maendeleo jumuishi nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...