BALOZI wa Shina Namba 8 la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kiburugwa Salumu Abdallah, yuko hoi kitandani kwa mwaka mmoja sasa baada ya nyumba yake kusombwa na mafuriko ya Mfereji wa Shego, ulipo katika kata hiyo wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke, Hamis Slim, akiongozana na Diwani wa kata hiyo, Rashid Chaburuma pamoja naq viongozi wa Chama, walifika nyumbani kwa Salumu kumjulia hali ambapo ameeleza bado anasumbuliwa na maradhi tangu nyumba yake iliposombwa na maji na kuomba jitihada za kutatua kero hiyo zifanyike.

Slim, alimhakikishia balozi huyo kuwa dhamira kubwa ya kufika katika eneo hilo la Mfereji wa Shego ni baada ya kupokea malalamiko mengi ya wanachama wa CCM, jumuia ya wazazi na wananchi kuhusu adha wanayoipata hasa kipindi cha mvua kutokana na mfereji huo kwa miaka mingi sasa.

“Tumefika hapa kukupa pole kwa sababu ulikuwa mstari wa mbele kueleza kuhusu changamoto ya mfereji huu. Chanzo cha maradhi yako ni baada ya kupata adha ya mafuriko na miongoni mwa nyumba zilizo sombwa ni nyumba yako. Tunakupa pole na tutaendelea kupambana kuhakikisha serikali yetu sikivu tunaishauri kumalizia sehemu ya iliyobaki ya ujenzi wa mradi huo,”amesema Slimu.

Ameeleza awali mfereji huo ulianza kutengenezwa katika Kata ya Charambe na kuishia katika Kata ya Kiburugwa lakini haukumaliziwa hadi Kata ya Mbagala ambapo unaishia Mto Mzinga.

Slimu amesema mvua kubwa iliyoinyesha mwaka jana na mwaka juzi ilisababisha mafuriko yaliyoondoka na nyumba nyingi za wakati wa eneo hilo.

“Ninaamini serikali ya CCM< chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ipo katika utaratibu wa kuboresha mazingira hususan miundombinu. Wananchi wawe watulivu kwa sababu Rais anaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa ndani ya siku 100,”amesema Slim.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Kiburugwa, Rashid Chabruma, amesema serikali imejipanga kuendeleza ujenzi na ujenzi wa mfereji huo hadi kwa Manganya ambapo jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa na Mbunge wa Mbagala Bruchad Kakulu .

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kingugi, Kata ya Kiburugwa, Athumani Magenge, ameeleza Mfereji wa Shego umekuwa adha kubwa kwa wananchi wa Mitaa ya Kingugi, Kwa nyoka na Magenge.

“Eneo hili limeaghiri zaidi ya kaya 300. Wengi walihifadhiwa katika ofisi zetu kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya mvua kubwa kunyesha mwaka jana na mwaka juzi. Zimebaki kilometa tano tu kumalizia ujenzi wa mfereji huyo. Mfereji huu unaendelea kutanuka na kuathiriwa,”amesema.

Ameiomba serikali kuwafikiria wananchi wa Kiburugwa kujenga mfereji huo ili kunusuru wananchi na kuondokana na adha kubwa wanayoipata mvua inapo nyesha.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...