Helakumi  Kacheri mkazi wa kitongoji cha Tindegela Kata ya Singisa Wilaya ya Morogoro anatafutwa na jeshi la polisi Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya mke wake kwa kutumia kitu chenye ncha kali. 

Kwa mujjibu wa Kamanda wa polisi mkoani hapa SACP Alex Mkama tukio hilo limetokea Januari 4 majira ya mchana wakati wawili hao wakiwa shambani.

Mkama alisema mtuhumiwa alimshambulia mkewe Sofina Alipisini (27) mkulima na mkazi wa Tendekela na kitu chenye makali sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda Mkama alisema mtuhumiwa alimtuhumu marehemu kuendeleza mahusiano ya karibu na mzazi mwenzie wa awali.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa huyo alitoroka mara baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Wakati huo huo polisi mkoani Morogoro inafanya uchunguzi juu ya vifo vya watu wawili vilivyotokea Wilaya ya Mvomero na Kilombero mkoani hapa.

Alisema tukio la kwanza lilmetokea januari 4 majira ya asubuhi katika kitongoji cha Isago Kata ya Mngeta Wilayani Morogoro ambapo Jese Melumba (49) mkazi wa Isago alikufa akidhaniwa kunywa sumu ya kuulia magugu ya shambani. 

Kamanda huyo alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwepo kwa mabaki ya dawa ya kuulia magugu iitwayo Banafos.

Katika tukio la pili lililotokea Januari 3 katika kitongoji cha Doma stendi, kilichopo kijiji na Kata ya Doma ambapo Ally Charles Dagaza (38) mkulima na mkazi wa kijiji hicho alikufa akiwa shambani kwake baada ya kukanyagwa na mnyama Tembo wakati akilinda miche ya nyanya na zao la pilipili.

Hivyo jeshi hilo linatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kama kuna mtu mwenye taarifa zinazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa aliyetenda tukio la mauaji kwa kuziwasilisha polisi na hatua za kisheria kuchukuliwa.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...