BANK of Africa Tanzania (BoA) imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya Huduma ya Kifedha yaliyoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango yaliyofanyika katika viwanja vya Usagara vilivyopo jijini Tanga.

Yakiwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi,” malengo makuu ya maadhimisho hayo yalikuwa ni kuongeza uelewa, kuboresha ufahamu na hatimaye kuhamasisha mabadiliko ya tabia za wananchi katika usimamizi wa fedha na matumizi ya huduma rasmi za kifedha.

Aidha, tukio hilo lililenga kuwahamasisha Watanzania kutumia huduma rasmi za kifedha kama sehemu ya jitihada za kupunguza kiwango cha umaskini katika jamii, ili kufikia maendeleo ya kiuchumi jumuishi na endelevu.
Maofisa uhusiano wa huduma za wateja wa Bank of Africa Tanzania, Ramadhan Nyamugumi na Gilbert John wakizungumza na wananchi waliotembelea banda la BoA katika maonesho hayo kwenye Uwanja wa Usagara, jijini Tanga
Washiriki wa Wiki ya huduma ya kifedha kitaifa wakiwa kwenye wakiwa kwenye Banda la Bank of Africa Tanzania (BoA) katika viwanja vya Usagara,jijini Tanga juzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...