Mkurungenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Bi. Erica Yegella amekutana na waandishi wa Habari jijini Mbeya kutoa taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu  ya sita katika kipindi cha siku 100  ndani ya halmashauri hiyo.

Ameyabainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari wilayni humo ambapo amesema lengo la  ni kuujulisha umma kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uboreshaji wa huduma za kijamii na kiuchumi katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Amesema kuwa katika kipindi cha oktoba 2025 hadi februari 2026 Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imepokea jumla ya shilingi bilioni 43.7 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali kati ya fedha hizo shilingi bilioni 38.4 zimetoka serikali kuu,zaidi ya milioni 767 kutoka kwa wadau  wa maendeleo huku zaidi ya shilingi bilioni 4.5 zikitokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.

Katika sekta ya afya Bi.Yegella amesema serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma kwa wananchi kwa kujenga na kukamilisha vituo vya afya na zahanati katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri.

Aidha Bi. Yegella amesema katika eneo la maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imeendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kiuchumi.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...