BENKI ya CRDB imezindua rasmi Ofisi yake ya Uwakilishi ya Dubai katika hafla iliyofanyika jana Dubai katika hoteli mashuhuri ya Intercontinetal, ikiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Balozi Kombo ameipongheza Benki ya CRDB kwa hatua hii muhimu akisema inaiweka Tanzania pamoja na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, uchumi wa pamoja unaokaribia dola za Marekani bilioni 800, moja kwa moja katika mfumo wa mitaji ya kimataifa, ikifanya Benki hiyokazi kama daraja kati ya fursa za kikanda na masoko ya fedha ya kimataifa.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema ofisi hiyo ya Dubai itatumika kama jukwaa la kimkakati la kuwezesha biashara, wawekezaji na pamoja na kuchochea upatikanaji wa mitaji ya kimataifa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na watu zaidi ya 700 wakiwamo viongozi wakuu wa Serikali, wawekezaji wa kimataifa, taasisi za fedha za kimataifa na washirika wa maendeleo. Ushiriki huu unaashiria kuongezeka kwa imani ya kimataifa kwa Benki ya CRDB kama daraja linaloaminika kati ya Afrika na masoko ya kimataifa.
#CRDBBank















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...