*Zimetengenezwa kwa kemikali bashirifu ili kukwepa sheria kukomesha dawa za kulevya
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KAMISHINA Msaidizi Sayansi Jinai kutoka Mamlaka ya Kudhibi na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Ziliwa Machibya amesema kuna dawa mpya za kulevya zaidi 1400 duniani ambazo zimetengenezwa kwa kutumia kemikamili bashirifu.
Dawa hizo za kulevya zinatengenezwa na wanaojihusisha na biashara hiyo kwa lengo la kukwepa sheria kwani dawa za kulevya ambazo zinakatazwa ziko katika orodha ya kisheria.
Machibya amesema hayo leo Januari 9,2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kilichoandaliwa na Mamlaka hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuwa na uelewa katika kupambana na dawa za kulevya nchini.
"Wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kukwepa masuala ya kisheria.Hivi sasa duniani kuna dawa mpya zaidi ya 1400 ambazo haziko katika orodha ya dawa zinazokatazwa."
Ameongeza kuwa dawa hizo mpya zinatengenezwa na watalaam ambao ni wabobezi wa sayansi na kwa kutumia kemikamili bashirifu viwandani na kutengeneza dawa hizo za kulevya.
"Siku hizi dawa nyingi zinatengenezwa kwa kemikamili bashirifu, hebu fikiria dawa za kulevya 1400 duniani haziko katika sheria lakini ni dawa za kulevya
Kuhusu kikao kazi hicho ametoa rai kwa waandishi wa habari nchini kuendelea kutoa taarifa za kuelimisha madhara yanayotokana ba marumizi ya dawa za kulevya huku akisisitiza umuhimu wa waandishi kufafuta taarifa katika vyanzo mbalimbali ili zifanyiwe kazi na mamlaka.
Kwa upande wake Moza Makumbuli ambaye ni Kamishina Msaidizi Kinga Huduma za Jamii kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya amesema katika kukomesha dawa za kulevya nchini Mamlaka imeendelea kutoa elimu kwa umma
“Mamlaka imekuwa na muongozo wa kuelimisha makundi mbalimbali na muongozo huo umeyagawa katika makundi 12 likiwemo kundi la vijana ambalo nalo limegawanywa katika makundi lengo kuhakikisha elimu inafika.
Amesema wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kufikisha elimu ya kukomesha dawa za kulevya ikiwemo kutumia klabu katika shuleni.
“Tunashirikiana na TAKUKURU kutoa elimu ya kupambana na dawa za kulevya kwasababu wao wanazo klabu nyingi ambazo wanazitumia kitoa elimu ya madhara ya rushwa, hivyo tunashirikiana katika mapambano dhidi ya dawq za kulevya.”
Kuhusu Mamlaka hiyo amesema inafanya kazi pia katika kanda na kupitia kanda hizo wanaendelea kutoa elimu ya madhara ya dawa za kulevya.
Hata hivyo ameeleza kuna kila sababu ya kuendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili wawe na uelewa mpana kuhusu dawa za kulevya.
Aidha amesema kuwa wamekuwa wakitumia vyomvoy vya habari kwa kiwango kikubwa lakini bado mamlaka haijatoa elimu y kutosha kwa vyombo vya habari.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...