Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, amefanikiwa kumaliza mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1,500 wa Kiwanda cha NAMERA kilichopo Gongolamboto, jijini Dar es Salaam, mgomo uliokuwa umeanza tarehe 16 Januari, 2026.
Mgomo huo ulitokana na madai ya mishahara, ambapo mshahara wa kima cha chini kwa sekta binafsi umewekwa kwa mujibu wa Tangazo na Amri ya Serikali Namba 605A ya tarehe 13 Oktoba, 2025, inayotoa ongezeko la wastani wa asilimia 33.4.
Kutokana na ongezeko hilo, mshahara wa chini umeongezeka kutoka Shilingi 275,060 mwaka 2022 hadi Shilingi 358,222 mwaka 2025. Hivyo basi, hakuna mtu au taasisi yoyote inayoruhusiwa kulipa mshahara chini ya kiwango kilichobainishwa katika Amri hiyo ya Serikali, hata kwa kuwepo kwa makubaliano yoyote kati ya taasisi binafsi kupitia chama chao cha waajiri (ATE) au mifumo mingine ya ndani.
Akizungumza na wafanyakazi pamoja na uongozi wa kiwanda hicho, Mhe. Mpogolo amesisitiza kuwa Amri ya Serikali ni ya lazima kutekelezwa na kwamba hakuna kampuni, taasisi au mwajiri yeyote anayekubalika kushuka chini ya viwango vilivyowekwa kisheria. Ameeleza kuwa makubaliano yoyote hayawezi kwenda kinyume na Amri ya Serikali.
Mpogolo ametoa maelekezo muhimu kwa uongozi wa kiwanda na wafanyakazi, ikiwemo kuhakikisha malipo ya mishahara yanatolewa kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 605A la mwaka 2025, huku akisisitiza kuwa hakuna mfanyakazi atakayefukuzwa kutokana na kushiriki mgomo, ili kuimarisha mahusiano bora kati ya mwajiri na waajiriwa. Aidha, ameitaka kiwanda kushirikiana na Chama cha Wafanyakazi (TUICO) na Afisa Kazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufanyika uchaguzi wa viongozi wa wafanyakazi watakao kuwa kiungo madhubuti kati ya wafanyakazi na uongozi, pamoja na kupitia mikataba ya ajira kuhakikisha inakidhi sheria na kanuni zinazohitajika. Mpogolo pia amehimiza ujenzi wa mahusiano mazuri na kulinda kiwanda kutokana na mchango wake mkubwa katika uchumi wa taifa na nafasi zake muhimu za ajira kwa wananchi.
Kwa upande wao, wafanyakazi wa kiwanda hicho wameeleza kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya, wakisema kuwa zimeleta matumain




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...