Serikali katika kata ya Nyanguku halmashauri ya manispaa ya Geita imetangaza vita dhidi ya wazazi ambao hawajawaandikisha watoto Elimu ya awali pamoja na waliofaulu kwenda kidato Cha kwanza.
Akizungumza na wazazi na Wanafunzi wakati wa zoezi la ugawaji wa madaftari kwa Wanafunzi wa shule za sekondari katika kata hiyo diwani wa Kata ya Nyanguku Elias Ngole ametamgaza operesheni ya kuwakamata wazazi ambao hawajawapeleka watoto shuleni tangu shule zilipofunguliwa.
Diwani wa kata ya Nyanguku Elias Ngole amekuwa na utaratibu wa kugawa madaftari kwa Wanafunzi wa shule za sekondari katika kata hiyo ambapo amesema kuwa zoezi hili ni sheria ya kata hiyo Kila diwani lazima atoe madaftari kwa Wanafunzi Kila mwaka.
Ngole ametoa onyo kwa wazazi ambao wamewafungia watoto bila kuwapeleka shule kwamba ifikapo jumatatu watakamatwa
"Kama una mtoto alitakiwa aende darasa la awali, darasa la kwanza na kama Kuna mtoto ambaye alitakiwa kuanza kitato Cha kwanza unae jumatatu tutashugulika na wewe" ameseema Ngole.
Kata ya Nyanguku inakabiliwa na changamoto ya utoro wa wanafunzi ambao unasababishwa na shughuli za kilimo zinazoendelea katika Kijiji hichi
Afisa Elimu katika kata hiyo Innocent Yasasa ametoa wito kwa wazazi katika kata hiyo kupeleka watoto shule ili waweze kupata haki yao ya msingi.
" Huku Kuna shughuli za kilimo zinazofanyika mfano, kipindi kama hiki Kuna kilimo Cha mpunga lakini pia Kuna kilimo Cha bustani za nyanya,vitunguu na mbogamboga kwahiyo wazazi wanawazuia watoto kwenda shule ili wahakilishe wanalima" alisema Innocent
Jumla ya Wanafunzi 135 wamepangiwa kidato Cha kwanza katika shule ya Sekondari Nyanguku ambapo mpaka Sasa ni Wanafunzi 90 TU ndio wamefika kuanza masomo.









Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...