Na Mwandishi wetu - Dodoma.
WAZIRI wa Nishati Deogratius Ndejembi anatarajia kuzindua kituo cha kupozea umeme cha Mtera ambacho kimejengwa kwa Fedha za Kitanzania shilingi bilioni 9.7.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy amesema kituo hicho kitasaidia kuongeza nguvu ya umeme hivyo kuwanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla.
Amesema awali kulikuwa na changamoto ya wananchi wa Dodoma na Mtera kupata umeme ambao hauna nguvu hivyo kituo hicho kitakuwa suluhisho.
“Mradi huu utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwani itaongeza nguvu ya umeme ambao unaweza kutumika kwa shughuli za kiuchimi ikiwemo viwanda vikubwa na vidogo,”alisema
Aliongeza kuwa :”Tunatarajia mradi huu uzinduliwe na waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi ambapo utanufaisha wananchi wa wilaya ya Mpwapwa na Kongwa na wale waishio vijiji vya Mtera,”
Katika hatua nyingine amesema Serikali inatarajia kusaini mkataba wa kusambaza umeme katika vijiji 9,009.
Mhandisi Saidy amesema mradi huo ni mkubwa ambao unafanya REA kutekeleza maono ya Rais Dk.Samia kuhakikisha vitongoji vyote vinafikiwa na huduma ya umeme.
“Huu ni mradi mkubwa ambao REA unaenda kutekeleza ukizingatia fedha itakayotumika ni kubwa.
Amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa miundombinu ya umeme ikiwemo nji za kusafirishia umeme zenye urefu wa kilometa 27,000, ufungaji wa trasifoma na kuwasha umeme katika vitongoji hivyo.
Vilevile amesema katika mradi huo watawaunganishia umeme watyeja wa awali 250,000 katika maeneo ambayo mradi huo utapita.
“Tukikamilisha mradi huu tutabakiwa na vitongoji 13,900 ambavyo vitakuwa havijaungwa na umeme. Kwa nia ambayo serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia imeonyesha tunatarajia vitongoji hibvi tuvimalizie kabla yam waka 2030,”
Aliongeza kuwa :“Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Afrika ambazo zimefanikiwa kufikisha miundombinu ya umeme katika vijiji vyote 12,318, Hivi sasa inaendelea na mpango mkakati wa kufikisha miundo mbinu ya umeme katika vitongoji vyote.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...