Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Dk.Asha-Rose Migiro ametoa mwito kwa viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo Wabunge na Mawaziri kushiriki katika vikao vya mashina na matawi vinavyoitishwa katika maeneo yao.
Akizungumza leo Januari 13 wakati akihitimisha ziara yake ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanya kikao kazi na viongozi wa CCM katika ngazi ya mashina pamoja na mabalozi Wilaya ya Ilala ameendelea kusisitiza umuhimu wa viongozi wa kitaifa wa Chama hicho kushiriki mikutano ya ngazi ya mashina na matawi.
“Tumesema mabalozi wetu mnafanya kazi nzuri kwani mnaitisha mikutano katika mashina yenu ,hivyo tunapenda kutoa mwito mikutano hii isiwe kwa watu ambao wako katika ngazi ya mashina peke yake au ngazi ya tawi peke.
“Viongozi wa kitaifa tunao wabunge katika mashina yetu , tunao mawaziri katika mashina yetu yetu.Nitoe mwito kwamba wawe sehemu ya mikutano hii kwasababu kwa hakika hakuna anayeanzia juu wote tunaanzia kwenye mashina yetu.
“Kwahiyo iwe ni mfano kwa viongozi wetu kuwa sehemu mikutano ile ambayo inaitishwa na mabalozi wetu kwa maana hiyo tutakwenda kadri tunavyoendelea baada ya kupata taarifa ,kupata muhatasari wa yale yanayoendelea tupate kujua ni namna gani tujiimarishe zaidi.
Amesisitiza viongozi wanaposhiriki kwenye vikao ndipo wanapata nafasi ya kutazama changamoto zinazowakabili kama chama lakini na changamoto zinazoikabili jamii yetu na Chama Cha Mapinduzi kina wajibu wa kuzichukua changamoto hizo na kuzifikisha kwenye ngazi za juu.
“Ili kwa pamoja na kwa kushirikiana nanyi mabalozi kwa kupata ushauri wenu kwa kupata nasaha zenu tuweze kuwapatia wananchi majibu ya changamoto zinazowakabili kwani wametupa dhamana ya uongozi
Kwa upande mwingine Dk.Migiro amezungumzia muelekeo wa Chama Cha Mapinduzi kimkakati katika kuendelea kuimarisha uhai wa chama hicho ambapo amefafanua mabalozi pamoja na kufanya kikao pia waendelee kuweka kumbukumbu za wanachama wao.
“Tumeambiwa hapa mashina ni sehemu muhimu sana ya usalama wa jamii yetu na usalama wa Taifa letu hivyo tutakuwa na wajibu wa kuhakikisha watu ambao tunaishi nao tunajua wanafanya nini na tunajua yale wanayoyafanya yanakuwa salama kwa Taifa letu
“Tunajua pia hivi sasa balozi wa shina anaweza kuwa na nyumba nyingi sana hivyo kupitia vikao vyetu tutaangalia ni namna gani balozi wa shina apate mzigo ambao anaweza kuubeba ili twende kwa pamoja kuhakikisha chama chetu kinaendelea kuwa chama kiongozi na kinaendelea kushika dola kwa manufaa ya taifa letu.”























Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...