-Asisitiza mabalozi kupandisha bendera za chama kwenye maeneo yao.
-Asema chama kinawajali na kuwathamini mabalozi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amesema maendeleo ya kweli kwa wananchi huanzia katika mashina ya Chama hicho, akisisitiza kuwa jitihada zote za maendeleo ya kijamii na kiuchumi hupata nguvu kupitia uongozi wa ngazi za chini.
Dkt. Migiro ambaye ni Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke tangu chama hicho kianzishwe, amesema hayo katika mkutano wake na Mabalozi wa Mashina wa CCM katika Wilaya ya Ilala, ikiwa ni hitimisho la ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam yenye lengo la kuimarisha uhai wa CCM kuanzia kwenye mashina Kwa kauli mbiu ya "Shina lako linakuita".
Akizungumza na Mabalozi hao amesema mashina ndiyo sehemu ya kwanza ya wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo, kwa kuwa ndiko wanakotoka wananchi wenyewe na ndiko changamoto zao halisi zinapojadiliwa.
Ameeleza kuwa mahusiano kati ya maendeleo ya jamii na maendeleo ya kisiasa hayawezi kutenganishwa, kwa kuwa mashina imara huwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji, jambo linaloongeza imani ya wananchi kwa Chama.
Ameongeza kuwa viongozi wa mashina wana wajibu mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao, akisema uangalizi wa karibu wa miradi hiyo ndio msingi wa maendeleo yenye tija kwa wananchi.
Aidha, Mwanadiplomasia huyo, amesema Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongeza kazi kubwa inayofanywa na mabalozi hao wa mashina na kwamba chama kitaendelea kuthamini mchango wao mkubwa kwenye mashina.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...