Na Mwandishi Wetu,TANGA

KATIBU MKUU wa Taifa wa Chama cha NLD Doyo Hassan Doyo leo January 6 mwaka huu 2026 ameongoza kikao cha Tathimini ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka 2025 cha Watendaji wa Makao Makuu na Afisi Kuu pamoja na Wagombea Wote.

Wagombea hao ni waliogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, ikiwa ni maandalizi ya vikao vya kikatiba vinavyotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Katika kikao hicho kimepitisha pia Taarifa ya maandalizi ya kugombea Ubunge Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma wakati tume itapotangaza rasmi kuanza mchakato wa kumpata mwakilishi wa Jimbo hilo .

Katibu Mkuu huyo aliwashukuru  wananchi wote waliokiunga mkono chama chetu katika kampeni zake nchin kote wakati wa uchaguzi mkuu.

Hata hivyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru  wagombea wote waliogombea nafasi mbalimbali kote nchini nakuwataka wasife moyo na kujipanga kisawasawa katika chaguzi zijazo katika nchi yetu kwani hiyo ndyo njia pekee ya kuweza kushika Dola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...