SERIKALI ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Finland zimesaini hati ya makubaliano ya kikanda [MoU] chini ya Mradi wa Maendeleo ya Matumizi ya Ardhi na Minyororo ya Thamani ya Misitu Tanzania [FORLAND] ili kuimarisha usimamizi na uratibu wa mandhari ya misitu katika mikoa ya Ruvuma na Lindi.
Hatua hii inakuja muda mfupi tu baada ya makubaliano kama haya kusainiwa na viongozi wa Mikoa ya Njombe na Iringa ambapo Forland inaendesha miradi ya usimamizi na uratibu wa misitu.
Mradi huu utatekelezwa katika nyanja tofauti zikiwemo za uzalishaji wa mbegu bora za miti,mikakati ya mapambano ya moto na utoaji elimu kwa wakulima wa miti.
Mratibu wa mradi wa FORLAND kutoka Wizara ya Maliasili na utalii Emma Nzunda alitumia fursa hiyo kusisitiza mashirikiano ya karibu kati ya pande zote za utekelezwaji wa mradi huo.
Mshauri mkuu wa kiufundi wa mradi wa FORLAND kutoka Nchini Finland, Michael Howkes amesema mradi huo utahusisha mnyororo mzima wa zao la misitu kuanzia wakulima wenyewe,wasafirishaji viwanda vya uchakataji pamoja na kuwajengea uwezo wadau wa misitu.
Naye Katibu Tawala wa MKoa wa Ruvuma, Joseph Martin na Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Kiuchumi na Uzalishaji Mkoa wa Lindi, Mwinjuma Mkungu kwa pamoja walikiri kuwapo kwa majanga ya moto yanayowarudisha nyuma wakulima na uchumi hivyo hatua hii ya kusaini makubaliano utasaidi kutatua changamoto hizi kwa urahisi.
Kwa upande wao wadau wa misitu nchini wamesema mradi huo uwanasue wakulima wa mitu kwenye madhira mbalimbali wanayokumbana naye hususani kwenye upande wa mbegu feki na majanga ya moto.
Kusainiwa kwa Mkataba huu kuna akisi dhamira ya pamoja ya wadau wote katika kukuza mandhari endelevu ya misitu,kuboresha maisha ya wananchi na kuchangia katika malengo ya kitaifa na kimataifa ya tabianchi na uhifadhi wa banuwai.
Shughuli hii ya utiaji saini pia ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa misitu na mazingira kutoka mikoa ya Ruvuma na Lindi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...