📍 BoT yaagizwa kudhibiti mikopo ya kausha damu
Na MASHAKA MHANDO, Tanga
TANZANIA imepata mafanikio makubwa kimataifa baada ya Umoja wa Ulaya (EU) kuiondoa rasmi nchi hiyo kwenye orodha ya nchi hatarishi kifedha (High-Risk List), hatua inayothibitisha kuimarika kwa mifumo ya udhibiti wa utakasishaji fedha na imani ya wawekezaji duniani.
Kufuatia mafanikio hayo ya kitaifa, Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Deogratius Luswetura, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuongeza udhibiti wa sekta ya fedha nchini ili kuwalinda wananchi dhidi ya taasisi zisizo rasmi zinazotoa mikopo umiza, maarufu kama "Kausha Damu", ambayo imekuwa ikisababisha watu kupoteza mali zao.
IMANI YA KIMATAIFA NA FATF
Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa jijini Tanga, Naibu Waziri amebainisha kuwa kuondolewa kwa Tanzania kwenye orodha hiyo (baada ya kuondolewa pia kwenye FATF Grey List mwishoni mwa 2025), kutarahisisha miamala ya kifedha kati ya Tanzania na nchi za Ulaya kuanzia Januari 29, 2026.
"Hatua hii inafungua milango mipya ya uwekezaji, inaongeza ushindani wa bidhaa zetu kimataifa na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu salama cha biashara barani Afrika," alisema Naibu Waziri.
CHANGAMOTO NA MAAGIZO KWA BoT
Pamoja na mafanikio hayo, Deogratius alikiri kuwepo kwa changamoto ya uelewa mdogo wa masuala ya fedha na uandishi wa maandiko ya miradi miongoni mwa Watanzania.
Alisisitiza kuwa Serikali haitavumilia wakopeshaji holela wanaowaumiza wananchi.
"Naiagiza BoT kuongeza udhibiti ili kuwaepusha wananchi na madhara ya kukopa katika taasisi zisizo rasmi. Wananchi pia mnaaswa kujiridhisha na uhalali wa taasisi na kuisoma mikataba vizuri kabla ya kusaini ili kuepuka hasara," alionya.
MAPINDUZI YA SEKTA YA BIMA
Akitoa salamu za Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Naibu Kamishna wa Bima, Khadija Said, alisema sekta hiyo imepiga hatua ambapo idadi ya watoa huduma imeongezeka kwa 26.5% hadi kufikia 1,741, huku wanufaika wakifikia Milioni 25.9.
Alibainisha kuwa uandikishaji wa ada za bima umekua kwa 20% hadi kufikia Trilioni 1.52, huku madai yaliyolipwa kwa wananchi yakiwa ni Bilioni 545.3.
UCHUMI WA TANGA UKO JUU
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dadi Kolimba, alibainisha kuwa pato la mkoa wa Tanga limekua kwa kasi kutoka Shilingi Trilioni 6.8 mwaka 2020 hadi kufikia Shilingi Trilioni 9.3 mwaka 2024.
Kolimba aliongeza kuwa pato la mwananchi mmoja mmoja mkoani Tanga nalo limepanda kutoka Shilingi Milioni 2.7 mwaka 2020 hadi kufikia Shilingi Milioni 3.4 mwaka 2024, jambo linaloashiria kuimarika kwa maisha ya wana-Tanga.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...