Na.Ashura Mohamed -Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Bw.Joseph Modest Mkude amewataka wananchi wa Wilaya ya Arusha Mjini kuhakikisha kuwa wanajenga tabia ya kufanya Usafi wa mazingira katika Maeneo yao wanayoishi.
Mkude amesema kuwa ikiwa kila mwananchi atafanya Usafi katika Maeneo yake ni wazi kuwa Maeneo mengi ya Wilaya ya Arusha yatakuwa safi na Jiji la Arusha litaendelea kung'ara kitaifa kwenye eneo la Usafi wa Mazingira.
Ameyasema hayo leo katika muendelezo wa kampeni ya Usafi wa Mazingira yenye kauli mbiu isemayo," Ng'arisha Jiji la Arusha"iliyozinduliwa na Mstahiki meya wa Jiji la Arusha mnamo Januari 02 na kuendelea leo katika hospital ya Wilaya ya Arusha iliyopo kata ya Engutoto.
"Usafi ni tabia ya mtu sasa tukianzia kufanya Usafi katika Maeneo yetu ni wazi kuwa itakuwa rahisi kwa mitaa yetu kuwa safi, hivyo kila mtu ajijengee mazoea haya ili Maeneo yake yawe safi tukiweza hivyo ni rahisi sana Maeneo ya Umma yatakuwa Safi tu"Amesisitiza Mkude
Aidha amesema kuwa Jiji lina uwezo wa kutosha kuhakikisha kuwa Halmshauri hiyo inashika nafasi ya kwanza kitaifa,katika Usafi wa mazingira,ambapo itakuwa Ajenda Mahususi kwa kuwa ni Jiji lenye Vivutio Vikubwa vya Utalii.
Pia amesisitiza kuwa swala la Usafi liende kwenye kata na kufanywa kwa Ushindani mkubwa ili kuwa na Matokeo chanya,ndani ya jamii kwa kuwa Usafi wa mazingira una faida kubwa ndani ya Jamii.
"Maeneo yasiwe hospitali tu kama hapa hapana,kuna Maeneo ya Umma kama mito,makorongo,Masoko haya yasisahaulike tupange muda tushirikishe watu ili kila kitu kuwa sawa nimefurahi pia mmesema mtaenda nyumba kwa nyumba"Amesema Mkude
Nae James Lobikoki ni Mkuu wa kitengo Cha Uthibiti wa Taka,na Usafi wa Mazingira Jiji letu la Arusha amesema kuwa kampeni hiyo ya Usafi ni muendelezo kuhakikisha kuwa Jiji linaendelea kung'ara,na kuhamasisha wananchi kwa kuona swalaa Usafi wa mazingira ni la kila mwananchi.
Hata hivyo ametoa rai kwa wazoa taka wa Jiji la Arusha kuendelea kufanya kazi hiyo kwa nguvu haswa katika kipindi hiki cha mvua za Vuli ili Maeneo ndani ya kataa yaendelee kuwa Safi na Salama.
Mratibu wa Kampeni hiyo ambaye ni diwani wa Viti Maalum bi.Aminata Salesh Toure,amesema awamu ya kwanza imeanza katika kata ya sokoni One katika eneo la Soko la dampo,Engutoto katika hospitali ya Wilaya na Kisha kumalizika katika soko la mbauda lililopo kata ya Sombetini kesho Januari 04,2025.
Bi.Salesh amesema kuwa madiwani wa Viti Maalum wamejipanga vema na kampeni hiyo itakwenda majumbani ili kuhakikisha wananchi wanashiriki zoezi kampeni hiyo na kuifanya Arusha kuwa salama na Safi.
Bw.Hamza Juma Njiku ni diwani wa kata ya Engutoto amesema kuwa kila Jumamosi watakuwa wanafanya Usafi katika Maeneo mbali mbali ndani ya kata hiyo kwa kuwa Usafi wa mazingira ni Ajenda ya Serikali inayoongizwa na Raisi daktari Samia Suluhu Hassan.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...