Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma (MNEC) Donald Mejetii, amesema serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeamua kurasimisha ajira zisizotambuliwa ili ziwe rasmi, hatua inayolenga kuwawezesha vijana waliyojiajiri kujikwamua kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza na wana-CCM wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kufungua Shina la Wakereketwa la CCM Jamuhuri Stadium, Januari 29, ikiwa ni  uzinduzi wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM, amesema chama kina imani kuwa vijana hao waliojiajiri watakuwa mabalozi wazuri wa kukitambulisha chama katika maeneo yao kwa lugha nzuri na matendo mema.

Ameeleza kuwa tawi hilo ni shina la kimkakati kutokana na eneo lake kupokea wageni wengi, hivyo lina nafasi kubwa ya kuitangaza CCM na sera zake kwa wananchi na wageni wanaofika katika eneo hilo.

Akizungumzia suala la mikopo kwa vijana, wanawake na makundi maalum amesema ni sera ya CCM inayotekelezwa na Serikali yake kupitia ilani ya uchaguzi, kwa lengo la kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi na kuongeza uzalishaji.

Aidha ameeleza kuwa Serikali ya CCM imerahisisha masharti ya mikopo ili wengi zaidi waweze kunufaika, akisisitiza kuwa mikopo hiyo itumike kwa malengo yaliyokusudiwa na irejeshwe kwa wakati ili iwanufaishe na wengine.

Amewataka wana-CCM kuendelea kushikamana, kudumisha umoja na kumpa ushirikiano Rais Samia Suluhu Hassan katika kupeperusha bendera ya chama na kusimamia maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbanga, amesema maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM Kimkoa yamezinduliwa rasmi mkoani humo kwa zoezi la upandaji miti, yakibeba kauli mbiu isemayo “Tumechagua umoja na amani kwa maendeleo ya taifa letu”, huku maadhimisho hayo yakitarajiwa kuhitimishwa Februari 5, 2026 Wilayani Chemba, ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emanuel Nchimbi.

Naye Said Rashid, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Uhuru, amewaasa vijana kuacha kusikiliza maneno ya watu wenye lengo la kupotosha mazuri yanayofanywa na chama badala yake wajikite kuangalia mazuri na fursa zinazopatika, kutokana na sera nzuri na madhubuti za chama hicho ikiwemo mikopo na ajira kwa vijana.

Kupitia maadhimisho ya miaka 49 ya CCM, chama kinaendelea kuimarisha mshikamano wa wanachama wake na kuhimiza ushiriki wa wananchi katika maendeleo ya taifa, huku kikisisitiza uwajibikaji, uzalendo na ushirikiano kwa maendeleo ya Tanzania.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...