Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC) pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wamekutana katika kikao kazi kilicholenga kutafuta suluhisho la changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika jimbo la Kibamba.
Akizungumza katika kikao hicho, Mbunge wa Kibamba, Mheshimiwa Angella Kairuki, amesema changamoto ya maji imekuwa kero kubwa kwa wananchi wa Jimbo hilo, hali inayohitaji hatua za haraka na za kudumu ili kuboresha upatikanaji wa huduma hiyo.
Amesema kuna umuhimu wa kuwa na chanzo zaidi ya kimoja katika Jimbo hili, hivyo kazi ya kutambua na kupata maeneo ya uchimbaji wa visima vya maji inabidi ifanyike ikiwa ni mkakati wa kuongeza vyanzo vya maji na kupunguza utegemezi wa miundombinu ya sasa.
“Kipaumbele chetu ni kutambua maeneo sahihi ya kuchimba visima vya maji ili kuongeza vyanzo vya maji na kupunguza adha kwa wananchi, kwa sababu tutakapokuwa na vyanzo vingine vya huduma ni vigumu sana wananchi kulalamika kwa muda mrefu juu ya ukosefu wa maji,” amesema Mheshimiwa Kairuki.
Mheshimiwa Mbunge amesema utekelezaji wa mpango wa uchimbaji wa visima vya maji, sambamba na maboresho ya mtandao wa usambazaji wa maji, utawezesha wananchi kupata huduma ya maji kwa uhakika, hasa katika maeneo yenye changamoto kubwa.
“Nawaomba watendaji wa DAWASA kuhakikisha maeneo ya uchimbaji wa visima yanapatikana kwa haraka ili utekelezaji wake uanze na kuondoa adha hii kwa wananchi,” amesema Mheshimiwa Kairuki ambaye pia ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na DAWASA ili kuhakikisha changamoto ya huduma ya maji katika Jimbo la Kibamba inapatiwa ufumbuzi wa kudumu na inaunga mkono juhudi zote za kitaalamu zitakazolenga kuboresha upatikanaji wa maji kwa wananchi.
Kwa niaba ya watendaji wa DAWASA katika jimbo la Kibamba, Ndugu Tumaini Mhondwa amesema tayari wanafanya tathmini ya kitaalamu ya maeneo mbalimbali kwa lengo la kubaini vyanzo vipya vya maji, ikiwemo uchimbaji wa visima, pamoja na kuboresha miundombinu ya usambazaji wa maji ili kuimarisha huduma ya maji katika jimbo hilo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...