Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv

VIJANA nchini wameungana kuadhimisha Siku ya Kumbukizi ya kuzaliwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakisema kuwa ni kiongozi mlezi wa vijana na chachu ya maendeleo ya taifa kwa vitendo.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo Januari 27,2026 Mratibu wa Taasisi ya Together for Samia ambaye pia ni Muandaaji wa shaghuli hiyo, Gulatone Masiga amesema tukio hilo limeandaliwa na vijana kwa hiari yao kama ishara ya upendo, heshima na kuthamini mchango wa Rais Samia katika kuwekeza maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla.

“Tuliona tufanye shughuli itakayotuleta pamoja, ikiwa ni nafasi ya sisi vijana kuonyesha upendo wetu kwa Rais wetu mama na mlezi wa vijana, ambaye ametujali na kuwekeza kwa vitendo katika maendeleo yetu,” amesema Masiga

Amesema vijana wengi waliokuwepo ni wa kizazi kipya ambacho kimenufaika kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Rais Samia katika kipindi cha takribani miaka mitano, hususan kupitia ujenzi wa vyuo vya ufundi na ujuzi katika zaidi ya wilaya 62 nchini, hatua iliyowezesha vijana kupata maarifa na ujuzi wa kujiajiri.

Masiga ameongeza kuwa mageuzi katika sekta ya elimu kupitia mtaala unaozingatia maarifa (knowledge-based curriculum) umehakikisha wahitimu wa elimu ya msingi na sekondari wanapata vyeti vya elimu ya kawaida sambamba na vyeti vya ufundi (VETA), hali inayowawezesha kuingia kwenye soko la ajira au kujiajiri.

Katika sekta ya nishati, amesema uwekezaji mkubwa wa serikali, ikiwemo mradi wa zaidi ya shilingi trilioni moja wa kupeleka umeme katika vitongoji 99 nchi nzima, umefungua fursa nyingi za kiuchumi kwa vijana, wakiwemo mafundi seremala, welders, wajasiriamali wa saluni, car wash na shughuli nyingine za uzalishaji.

“Tunaona wazi kwamba uwekezaji huu ni fursa ya moja kwa moja kwa vijana,” amesema.

Ameeleza pia kuwa miradi mikubwa ya miundombinu ikiwemo reli ya kisasa (SGR) inayounganisha mikoa mbalimbali nchini itakapokamilika, vijana watakuwa miongoni mwa wanufaika wakuu kupitia ajira na shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wa sekta ya afya, vijana hao wamepongeza ujenzi wa vituo vya afya hadi ngazi ya kata pamoja na kuanza kwa mpango wa bima ya afya kwa wote, ambapo kaya zitalipia kiasi cha shilingi 150,000 kwa familia yenye watu sita, huku makundi maalum yakigharamiwa na serikali.

Mmoja wa vijana walioshiriki hafla hiyo, Dorcas Mshiu ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa muanzilishi wa Vijana Innovation, amesema Rais Samia amefungua fursa nyingi za kiuchumi kwa vijana, ikiwemo urahisishaji wa usajili wa biashara na kuvutia wawekezaji nchini.

“Mama yetu hajatuacha.

Amesema kuwa Rais Samia ametengeneza mazingira rafiki kwa vijana kujiajiri, ikiwemo mikopo ya asilimia mbili na nne kupitia halmashauri. Hii ni serikali inayowaamini vijana,” amesema Doras.

Vijana hao wamesema sababu ya kuadhimisha siku hiyo ni kutambua uongozi wa Rais Samia unaojengwa juu ya misingi ya maridhiano, amani na umoja wa kitaifa, wakiahidi kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya taifa.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...