Na MWANDISHI WETU

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ambaye ni Diwani wa Kata ya Kibada Mhe. 𝗔𝗺𝗶𝗻𝗶 𝗠𝘇𝘂𝗿𝗶 𝗦𝗮𝗺𝗯𝗼, amefanya ziara ya kuwatembelea, kuwajulia hali na kuwapa mahitaji maalumu (sabuni na fedha )  wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Gezaulole, leo  Januari Mosi 2026.

Akiwa hospitalini hapo, Mhe. Sambo ametumia fursa hiyo pia kusikiliza na kupokea changamoto za wagonjwa wananchi na wahudumu wa afya wa katika  hospitali hiyo.

Baadhi ya maombi  aliyopokea ni  mahitaji ni  kujengwa chumba maalumu cha kuhudumia wateja maalumu kwa wazazi wakiwa katika uangalizi maalumu.

Akizungumza na wagonjwa katika wodi ya wazazi, wanaume na watoto, Mhe. Sambo, amepokea salamu za shukrani kutoka kwao  ambapo wamemweleza  wazi kupewa huduma bora za afya.

Wamemwomba kufikisha salamu zao kwa Rais Dk.  Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha huduma za afya  kwani  licha ya kupatiwa huduma bora pia walisema hawajadaiwa fedha.

 “Utu  umetangulizwa kwa kweli Rais Dk. Samia  ameanza kutekeleza ahadi yake ya kuboresha huduma za afya ndani ya siku 100 za uongozi wake,”alisema mmoja wa wananchi.

Kwa upande wake  Mstahiki Meya Sambo amewekea msisitizo kuwa huduma hiyo bora  ya afya inayoendelea kutolewa isiishie ndani ya siku 100 tu za ahadi ya  Rais Dk. Samia na kuwatia moyo wauguzi  kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi. 

Pia, amebainisha, halmashauri itajipambanua katika kuongeza fedha za kutumika katika mahitaji ya ujenzi  wa miundombinu ya kutolea huduma  katika  hospitali hiyo.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni  Lucas David alimweleza meya huyo  kuwa wamepokea fedha sh.milioni 800 kutoka serikalini ambazo zitatumika kwa ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti na wodi mahususi kwa wagonjwa wa upasuaji ambapo ameeleza kuwa jengo hilo litakuwa la ghorofa 6.

Pia Dkt. Lucas amesema, hospitalini hapo wapo madaktari bingwa mahususi akiwemo wa huduma za akina mama na Daktari bingwa wa huduma za watoto.

Katika hatua nyingine, Mstahiki Meya Sambo amesema Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni itaiishi kwa vitendo hotuba ya kufunga mwaka iliyotolewa na Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮  katika kuingia mwaka huu wa 2026 na kuwatakia wananchi wote wa halmashauri hiyo heri ya mwaka mpya 2026.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...